029-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kumuadhibu Mtumwa na Mnyama na Mwanamke na Mtoto Bila ya Sababu ya Kisheria au Zaidi ya Kile Kiwango cha Kutia Adabu
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن تعذيب العبد والدابة
والمرأة والولد بغير سبب شرعي أَوْ زائد عَلَى قدر الأدب
029-Mlango Wa Kukatazwa Kumuadhibu Mtumwa na Mnyama na Mwanamke na Mtoto Bila ya Sababu ya Kisheria au Zaidi ya Kile Kiwango cha Kutia Adabu
قال الله تَعَالَى :
وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا ﴿٣٦﴾
Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa na rafiki wa karibu, na msafiri aliyeishiwa masurufu, na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. Hakika Allaah Hapendi mwenye majivuno mwenye kujifakharisha. [An-Nisaa: 36]
Hadiyth – 1
وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( عُذِّبَتِ امْرَأَةٌ في هِرَّةٍ سَجَنَتْها حَتَّى مَاتَتْ ، فَدَخَلَتْ فِيهَا النَّارَ ، لاَ هِيَ أَطْعَمَتْهَا وَسَقَتْهَا ، إذْ حَبَسَتْهَا ، وَلاَ هِيَ تَرَكَتْهَا تَأكُلُ مِنْ خَشَاشِ الأَرْضِ )) . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ameadhibiwa mwanamke kwa sababu ya paka aliyemfunga mpaka akafa, akaingizwa motoni kwa ajili ya jambo hilo, kwani alipomfunga hakumpa chakula wala hakumpa maji, na wala hakumwacha ale vijidudu vya ardhi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وَعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّهُ مَرَّ بِفِتْيَانٍ مِنْ قُرَيْشٍ قَدْ نَصَبُوا طَيراً وَهُمْ يَرْمُونَهُ ، وَقَدْ جَعَلُوا لِصَاحِبِ الطَّيْرِ كُلَّ خَاطِئَةٍ مِنْ نَبْلِهمْ ، فَلَمَّا رَأَوْا ابْنَ عُمَرَ تَفَرَّقُوا ، فَقَالَ ابْنُ عُمَرَ : مَنْ فَعَلَ هَذَا ؟ لَعَنَ اللهُ مَنْ فَعَلَ هَذَا ، إنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم لَعَنَ مَنِ اتَّخَذَ شَيْئاً فِيهِ الرُّوحُ غَرَضاً . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa walipita vijana wa Ki-Quraysh, wakiwa wamemshika ndege na wanamlenga shabaha. Hakika ni kuwa walikuwa wamepanga na mwenye ndege kuwa mishale yote itakayokosa shabaha itakuwa yake. Walipomuona Ibn 'Umar walikimbia. Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) akauliza: "Nani alifanya hivi?" Allaah Amlaani aliyefanya jambo hili. Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani yeyote anayelenga shabaha kitu chenye roho." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أنس رضي الله عنه قَالَ : نهى رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم أن تُصْبَرَ البَهَائِمُ . متفق عَلَيْهِ .
Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Amekataza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwanyima wanyama chakula mpaka wafe." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أَبي عليٍّ سويدِ بن مُقَرِّنٍ رضي الله عنه قَالَ : لَقَدْ رَأَيْتُنِي سَابِعَ سَبْعَةٍ مِنْ بَنِي مُقَرِّنٍ مَا لَنَا خَادِمٌ إِلاَّ وَاحِدَةٌ لَطَمَهَا أصْغَرُنَا فَأَمَرَنَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم أنْ نُعْتِقَهَا . رواه مسلم .
وفي روايةٍ : (( سَابعَ إخْوَةٍ لِي )) .
Amesema Abu 'Aliy Suwayd bin Muqarrin (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilikuwa mimi mmoja katika watu saba wa ukoo wa Bani Muqarrin na hatukuwa na mtumwa ila mmoja tu. Mdogo wetu kabisa alimpiga kofi, kwa ajili hiyo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituamuru tumuache huru. [Muslim].
Na katika riwaayah nyengine: "Nilikuwa na ndugu saba."
Hadiyth – 5
وعن أَبي مسعودٍ البدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ أضْرِبُ غُلامَاً لِي بالسَّوْطِ، فَسَمِعْتُ صَوْتاً مِنْ خَلْفِي : (( اعْلَمْ أَبَا مَسْعُودٍ )) فَلَمْ أفْهَمِ الصَّوْتِ مِنَ الغَضَبِ ، فَلَمَّا دَنَا مِنِّي إِذَا هُوَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ، فإذا هُوَ يَقُولُ : (( اعْلَمْ أَبَا مَسْعُودٍ أنَّ اللهَ أقْدَرُ عَلَيْكَ مِنْكَ عَلَى هَذَا الغُلامِ )) . فَقُلتُ : لا أضْرِبُ مَمْلُوكاً بَعْدَهُ أَبَداً .
وَفِي روايةٍ : فَسَقَطَ السَّوْطُ مِنْ يَدِي مِنْ هَيْبَتِهِ .
وفي روايةٍ : فَقُلتُ : يَا رسولَ الله ، هُوَ حُرٌّ لِوَجْهِ اللهِ تَعَالَى ، فَقَالَ : (( أمَا لَوْ لَمْ تَفْعَلْ ، لَلَفَحَتْكَ النَّارُ ، أَوْ لَمَسَّتْكَ النَّارُ )) . رواه مسلم بهذه الروايات .
Amesema Abu Mas'uwd Al-Badriy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilikuwa mara moja nikimpiga mtumwa wangu na koboko, nikasikia sauti nyuma yangu: "Tanabahi na ujue, ee Abu Mas'uwd." Sikufahamu sauti hiyo kwa ghadhabu nilizokuwa nazo. Alipofika karibu nami, ndipo nilipojua kuwa ni Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye alikuwa anasema: "Tanabahi na ujue, ee Abu Mas'uwd! Hakika Allaah ana uwezo na nguvu zaidi kuliko ulio nao juu ya mtumwa huyu." Nikamwambia: "Sitampiga mtumwa baada ya leo milele."
Na katika riwaayah nyengine: "Kiboko kikaanguka kutoka katika mkono wangu kwa haiba yake."
Na katika riwaayah nyengine: Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Huyu mtumwa wangu yupo huru kwa ajili ya kutaka radhi za Allaah Ta'aalaa." Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Lau hukufanya hivyo, ungechomwa katika moto au moto ungekugusa." [Muslim kwa riwaayah zote hizi].
Hadiyth – 6
وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ ضَرَبَ غُلاَمَاً لَهُ حَدّاً لَمْ يَأتِهِ ، أَوْ لَطَمَهُ ، فإنَّ كَفَارَتَهُ أنْ يُعْتِقَهُ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwake Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumuadhibu mtumwa wake kwa kumpiga au kumchapa kofi la uso bila ya makosa yoyote, kafara yake itakuwa ni kumuacha huru (mtumwa huyo)." [Muslim]
Hadiyth – 7
وعن هِشام بن حكيمِ بن حِزَامٍ رضي الله عنهما : أنَّه مَرَّ بالشَّامِ عَلَى أُنَاسٍ مِنَ الأَنْبَاطِ ، وَقَدْ أُقيِمُوا في الشَّمْسِ ، وَصُبَّ عَلَى رُؤُوسِهِمُ الزَّيْتُ ! فَقَالَ : مَا هَذَا ؟ قيل : يُعَذَّبُونَ في الخَرَاجِ - وفي رواية : حُبِسُوا في الجِزْيَةِ - فَقَالَ هِشَامٌ : أشهدُ لَسَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( إنَّ اللهَ يُعَذِّبُ الَّذِينَ يُعَذِّبُونَ النَّاس في الدُّنْيَا )) . فَدَخَلَ عَلَى الأمِيرِ ، فَحَدَّثَهُ ، فَأَمَرَ بِهِمْ فَخُلُّوا . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwake Hishaam bin Hakiym bin Hizaam (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa alipita Shaam (Syria) na akawaona watu wa Anbaat (masikini wakulima wasiokuwa Waislamu wala Waarau) waliokuwa wamesimamishwa kwenye jua na wakamiminiwa mafuta vichwani. Akasema (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Hii ni nini?" Akaambiwa: "Wanaadhibiwa ili waweze kutoa ushuru." Na katika riwaayah nyengine: "Wamefungwa kwa ajili ya kupata jizya kutoka kwao." Hishaam alisema: "Nashuhudia ya kwamba nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: 'Hakika Allaah Atawaadhibu wale ambao kwamba wanawaadhibu watu hapa duniani." Baada ya hapo alikwenda kwa Amiri na kumwelezea kuhusu Hadiyth hii. Amiri aliamuru watu hao waachiliwe (wasiwe ni wenye kuadhibiwa)." [Muslim]
Hadiyth – 8
وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : رأى رسولُ الله صلى الله عليه وسلم حِمَاراً مَوْسُومَ الوَجْهِ ، فَأَنْكَرَ ذَلِكَ ؟ فَقَالَ : (( واللهِ لا أسِمُهُ إِلاَّ أقْصَى شَيْءٍ مِنَ الوَجْهِ )) وأمَرَ بِحِمَارِهِ فَكُوِيَ في جَاعِرَتَيْهِ ، فَهُوَ أوَّلُ مَنْ كَوَى الجَاعِرَتَيْنِ . رواه مسلم .
Amesema Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona punda aliyekuwa ametiwa alama kwenye uso wake, alikataza jambo hilo na kuchukizwa sana. Akasema Ibn 'Abbaas: "Wa-Allaahi! Sitamtia alama punda wangu isipokuwa sehemu iliyo mbali sana na uso wake." Aliamuru punda wake aletwe na atiwe alama kwenye mapaja yake, hivyo akawa wa kwanza katika kutia alama punda kwenye mapaja. [Muslim]
Hadiyth – 9
وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم مَرَّ عَلَيْهِ حِمَارٌ قَدْ وُسِمَ في وَجْهِهِ ، فَقَالَ : (( لَعَنَ اللهُ الَّذِي وَسَمَهُ )) . رواه مسلم .
وفي رواية لمسلم أَيضاً: نهى رسول الله صلى الله عليه وسلم عَنِ الضَّرْبِ في الوَجْهِ ، وَعَنِ الوَسْمِ في الوَجْهِ
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa mara moja punda alipita mbele ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa ametiwa alama kwenye uso wake. Akasema: "Allaah Amlaani yule aliyemtia alama usoni mwake." [Muslim].
Na katika riwaayah ya Muslim: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kupigwa mnyama kwenye uso na kutiwa alama sehemu hiyo."