03-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Kuwinda Na Hukmu Zake: Njia Za Uwindaji: Njia Ya Kwanza
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الصَّيْدُ وَأَحْكَامُهُ
Kuwinda Na Hukmu Zake
03- Kuwinda Na Hukmu Zake: Njia Za Uwindaji: Njia Ya Kwanza
Uhalali wa kuwinda unamaanisha kumwezesha mwindaji kumkamata mnyama na kumdhibiti akiwa hai ikiwezekana, au akiwa ameuawa kwa zana ya kuwindia, kwa kuwa kumuua mnyama kwa zana ya kuwindia kunazingatiwa kuwa sawa na kumchinja chinjo la kisharia. Njia zote au ala zote za kuwindia zina masharti maalum ya kumfanya mnyama aliyeuawa kuwa kama amechinjwa chinjo la kisharia.
Njia Ya Kwanza Ya Uwindaji: Kuwinda Kwa Kutumia Wanyama Au Ndege Wakali
Wanyama wakali wakusudiwao hapa ni wale wenye meno makali ya kuulia kiwindwa kama mbwa, cheetah na kadhalika. Ama ndege, hawa ni wale wenye kucha kali za kuulia kiwindwa kama vile kozi, kipanga na kadhalika. Ni kwa Neno Lake Allaah Ta’aalaa:
"وَمَا عَلَّمْتُم مِّنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّـهُ"
“Na mlivyowindiwa na wanyama na ndege wakali mliowafundisha kiweledi, na mnawafunza katika ambayo Allaah Amekufunzeni”. [Al-Maaidah : 04].