052-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Uharamu wa Kuchora Wanyama katika Busati au Mawe, Nguo, Dirhamu, Dinari (Hela), Mto na Kadhalika na Uharamu wa Kuwa na Picha katika Ukuta, Pazia, Kilemba, Nguo na Mfano wake na Amri ya Kufuta Picha
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم تصوير الحيوان في بساط
أو حجر أو ثوب أو درهم أو مخدة أو دينار أو وسادة وغير ذلك
وتحريم اتخاذ الصور في حائط وسقف وستر وعمامة وثوب ونحوها
والأمر بإتلاف الصورة
052-Mlango Wa Uharamu wa Kuchora Wanyama katika Busati au Mawe, Nguo, Dirhamu, Dinari (Hela), Mto na Kadhalika na Uharamu wa Kuwa na Picha katika Ukuta, Pazia, Kilemba, Nguo na Mfano wake na Amri ya Kufuta Picha
Hadiyth – 1
عن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّ الَّذينَ يَصْنَعُونَ هذِهِ الصُّوَرَ يُعَذَّبُونَ يَوْمَ القِيامَةِ ، يُقَالُ لَهُمْ : أحْيُوا مَا خَلَقْتُمْ )) . متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: "Hakika wanaotengeneza hizi picha wataadhibiwa Siku ya Qiyaamah, wataambiwa vipeni uhai mlivyo viumba." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَدِمَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم مِنْ سَفَرٍ ، وَقَدْ سَتَرْتُ سَهْوَةً لِي بِقِرامٍ فِيهِ تَمَاثيلُ ، فَلَمَّا رَآهُ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم تَلَوَّنَ وَجْهُهُ، وقالَ: (( يَا عائِشَةُ ، أشَدُّ النَّاسِ عَذَاباً عِندَ اللهِ يَوْمَ القِيَامَةِ الَّذينَ يُضَاهُونَ بِخَلْقِ اللهِ ! )) قَالَتْ : فَقَطَعْنَاهُ فَجَعَلْنَا مِنهُ وِسَادَةً أوْ وِسَادَتَيْنِ . متفق عليه .
Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifika, kutoka safarini, akanikuta nimeweka pazia yangu yenye mapicha. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipoiona uso wake ulibadilika rangi na kusoma: "Ee 'Aaishah! Walio na adhabu kali kuliko watu wote Siku ya Qiyaamah ni wale wanaoiga umbile aliloliumba Allaah." 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) akasema: "Tukaikata, na tukafanya kutokana nayo mto, mmoja au miwili." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na An-Nisaaiy]
Hadiyth – 3
وعن ابن عباس رضي اللهُ عنهما ، قال : سمعتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( كُلُّ مُصَوِّرٍ في النَّارِ يُجْعَلُ لَهُ بِكُلِّ صُورَةٍ صَوَّرَهَا نَفْسٌ فَيُعَذِّبُهُ في جَهَنَّمَ )) . قال ابن عباس : فإنْ كُنْتَ لاَ بُدَّ فَاعِلاً ، فَاصْنعِ الشَّجَرَ وَمَا لاَ رُوحَ فِيهِ. متفق عليه.
Amesema Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Kila mwenye kutengeneza picha ataingizwa motoni, atajaaliwa kwa kila picha aliyochora nafsi itakayomuadhibu ndani ya Jahanamu." Akasema Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): "Na ikiwa huna budi ufanye (shughuli hiyo ya kuchora) basi tengeneza (picha ya) miti na vitu visivyokuwa na roho." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن ابن عباس رضي اللهُ عنهما ، قال : سمعتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَنْ صَوَّرَ صُورَةً فِي الدُّنْيَا ، كُلِّفَ أَنْ يَنْفُخَ فِيهَا الرُّوحَ يَومَ القِيَامَةِ وَلَيْسَ بِنَافِخٍ )) . متفق عليه .
Amesema Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kuchora picha ataadhibiwa na kukalifishwa kupuliza ndani yake uhai na hataweza kufanya hivyo." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 5
وعن ابن مسعودٍ رضي اللهُ عنه قال : سمعتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( إنَّ أشَدَّ النَّاسِ عَذَاباً يَومَ القِيَامَةِ المُصَوِّرُونَ )) . متفق عليه .
Amesema Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika aliye na adhabu kali zaidi ya wote Siku ya Qiyaamah ni watengeneza picha." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nisaaiy]
Hadiyth – 6
وعن أبي هريرة رضي اللهُ عنه قال : سمعتُ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( قال اللهُ تَعَالَى : وَمَنْ أظْلَمُ مِمَّنْ ذَهَبَ يَخْلُقُ كَخَلْقِي ؟ فَلْيَخْلُقُوا ذَرَّةً أوْ لِيَخْلُقُوا حَبَّةً ، أوْ لِيَخْلُقُوا شَعِيرَةً )) . متفق عليه .
Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Amesema Allaah Ta'aalaa: Hakuna aliye dhulumu zaidi ya yule anaye jaribu kuumba kama Nilivyoumba, basi ajaribu kuumba atomu (ni kitu kidogo sana ambacho hakiwezi kuonekana ila kwa ala ya kukuza kitu) au aiumbe chembe moja ya nafaka au aiumbe shayri." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 7
وعن أبي طلحة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( لاَ تَدْخُلُ المَلاَئِكَةُ بَيْتاً فيهِ كَلْبٌ وَلاَ صُورَةٌ )) . متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa Abu Twalhah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Malaaikah hawaingii nyumba iliyo na mbwa ndani yake wala iliyo na picha au masanamu." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawud, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah].
Hadiyth – 8
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قال : وَعَدَ رسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم جِبْرِيلُ أنْ يَأتِيَهُ ، فَرَاثَ عَلَيْهِ حَتَّى اشْتَدَّ عَلَى رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فَخَرَجَ فَلَقِيَهُ جِبريلُ فَشَكَا إلَيهِ ، فَقَالَ : إنَّا لاَ نَدْخُلُ بَيْتاً فِيهِ كَلْبٌ وَلاَ صُورَةٌ . رواهُ البُخاري .
Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Mara moja Jibriyl aliahidi kumzuru Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) lakini alichukua muda mrefu mpaka likamkera Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) jambo hilo. Alipotoka nyumbani kwake alikutana na Jibriyl na kumlalamikia kuhusu hilo. Akasema Jibriyl: "Hakika sisi hatuingii nyumba iliyo na mbwa ndani yake wala iliyo na picha au masanamu." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 8
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : واعدَ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، جبريلُ عليهِ السَّلامُ ، في سَاعَةٍ أنْ يَأتِيَهُ ، فَجَاءتْ تِلْكَ السَّاعَةُ وَلَمْ يَأتِهِ ! قَالَتْ : وَكَانَ بِيَدِهِ عَصاً، فَطَرَحَهَا مِنْ يَدِهِ وَهُوَ يَقُولُ : (( ما يُخْلِفُ اللهُ وَعْدَهُ وَلاَ رُسُلُهُ )) ثُمَّ التَفَتَ ، فإذَا جَرْوُ كَلْبٍ تَحْتَ سَرِيرِهِ . فقالَ : (( مَتَى دَخَلَ هَذَا الكَلْبُ ؟ )) فَقُلْتُ : واللهِ مَا دَرَيْتُ بِهِ ، فَأمَرَ بِهِ فَأُخْرِجَ ، فَجَاءهُ جِبْرِيلُ (عَلَيْهِ السَّلام) ، فقال رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( وَعَدْتَنِي، فَجَلَسْتُ لَكَ وَلَمْ تَأتِني )) فقالَ : مَنَعَنِي الكَلْبُ الَّذِي كانَ في بَيْتِكَ ، إنَّا لاَ نَدْخُلُ بَيْتاً فِيهِ كَلْبٌ وَلاَ صُورَةٌ . رواه مسلم .
Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Mara moja Jibriyl alimuahidi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa atamtembelea baada ya muda (usiku). Jibriyl hakufika wakati huo wa miadi. Akasema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na fimbo mkononi mwake ambayo aliitupa, huku anasema: 'Allaah Hakhalifu ahadi Yake wala wajumbe Wake'." Kisha akatizama na kumuona mbwa chini ya kitanda chake cha mbao, na hapo akauliza: "Mbwa huyu ameingia lini?" Nikasema: "Wa-Allaahi! Sikumuona kabisa akiingia." Akaamuru atolewe, naye akatolewa. Jibriyl alikuja wakati huo, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: 'Uliniahidi kuwa utanizuru, nami nimekataa kukungojea lakini hukufika." Akasema: "Amenizuia mimi yule mbwa aliyekuwa ndani ya nyumba yako. Hakika sisi hatuingii nyumba iliyo na mbwa ndani yake wala iliyo na picha au masanamu." [Muslim]
Hadiyth – 9
وعن أبي الهَيَّاجِ حَيَّانَ بِن حُصَيْنٍ ، قال : قال لي عَليُّ بن أبي طالب رضي اللهُ عنه : ألاَ أبْعَثُكَ عَلَى مَا بَعَثَنِي عَلَيْهِ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ؟ أن لاَ تَدَعَ صُورَةً إلاَّ طَمَسْتَهَا ، وَلاَ قَبْراً مُشْرفاً إلاَّ سَوَّيْتَهُ . رواه مسلم .
Amesema Abil Hayyaaj Hayyan bin Huswayn: Aliniambia mimi 'Ali bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Je, sikutumi kwa alilonituma kwayo Rasuli wa Allaah? Usiache picha yoyote isipokuwa umeifutilia mbali (au sanamu isipokuwa umelivunja) wala kaburi lolote ambalo limenyanyuliwa isipokuwa umelisawazisha." [Muslim]