054-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kuwafunga Kengele Ngamia na Wanyama Wengine na Ukaraha wa Kumchukua Mbwa na Kengele katika Safari
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهية تعليق الجرس في البعير وغيره من الدواب
وكراهية استصحاب الكلب والجرس في السفر
054-Mlango Wa Ukaraha wa Kuwafunga Kengele Ngamia na Wanyama Wengine na Ukaraha wa Kumchukua Mbwa na Kengele katika Safari
Hadiyth – 1
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَصْحَبُ المَلاَئِكَةُ رُفْقَةً فِيهَا كَلْبٌ أوْ جَرَسٌ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Malaaikah wa rehma hawafuati msafara ulio na mbwa au kengele." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أبي هريرة رضي الله عنه قال : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( الجَرَسُ مَزَامِيرُ الشَّيْطَانِ )) . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kengele ni katika zumari za shetani." [Muslim]