056-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kutema Mate Msikitini, Amri ya Kuyaondoa Yanapopatikana na Amri ya Kusafisha Msikiti
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النهي عن البصاق في المسجد
والأمر بإزالته منه إذا وجد فيه
والأمر بتنـزيه المسجد عن الأقذار
056-Mlango Wa Kukatazwa Kutema Mate Msikitini, Amri ya Kuyaondoa Yanapopatikana na Amri ya Kusafisha Msikiti
Hadiyth – 1
عن أنس رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( البُصاقُ في المَسْجِدِ خَطِيئَةٌ ، وَكَفَّارَتُهَا دَفْنُهَا )) . متفق عليه .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kutema mate Msikitini ni kosa na kafara lake ni kuyafukia." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم رَأَى في جِدَارِ القِبْلَةِ مُخَاطاً ، أَوْ بُزَاقاً ، أَوْ نُخَامَةً ، فَحَكَّهُ . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliona katika ukuta wa Qiblah kamasi, au mate, au kohozi, akalikwangua." [Al-Bukhaariy, Muslim na Maalik]
Hadiyth – 3
وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ هذِهِ المَسَاجِدَ لاَ تَصْلُحُ لِشَيءٍ مِنْ هَذَا البَوْلِ وَلاَ القَذَرِ ، إنَّمَا هي لِذِكْرِ اللهِ تَعَالَى ، وَقِراءةِ القُرْآنِ )) أَوْ كَمَا قَالَ رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika haifai kuitumia Misikiti kwa ajili ya kukojoa ndani yake wala kuichafua (kwa kuitia najisi). Hakika hiyo Misikiti ni kwa ajili ya kumdhukuru Allaah Ta'aalaa na kusoma au kama alivyosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." [Muslim]