066-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Mtu Kuomba kwa Jina la Allaah Mbali na Jannah na Ukaraha wa Kumkataza Mwenye Kuomba kwa Allaah Ta'aalaa
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة أنْ يسأل الإنسان بوجه الله عزوجل
غير الجنة ، وكراهة منع من سأل بالله تعالى وتشفع به
066-Mlango Wa Ukaraha wa Mtu Kuomba kwa Jina la Allaah Mbali na Jannah na Ukaraha wa Kumkataza Mwenye Kuomba kwa Allaah Ta'aalaa
Hadiyth – 1
عن جابر رضي الله عنه قالَ : قالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ يُسْأَلُ بِوَجْهِ اللهِ الا الجَنَّةُ )) . رواه أبو داود .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakiombwi kwa jina la Allaah ila Jannah." [Abu Daawuwd]
Hadiyth – 2
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قال : قال رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنِ اسْتَعَاذَ بِاللهِ ، فَأعِيذُوهُ ، وَمَنْ سَأَلَ بِاللهِ ، فأَعْطُوهُ ، وَمَنْ دَعَاكُمْ ، فَأَجِيبُوهُ ، وَمَنْ صَنَعَ إلَيْكُمْ مَعْرُوفاً فَكَافِئُوهُ ، فَإنْ لَمْ تَجِدُوا ما تُكَافِئُونَهُ بِهِ فَادْعُوا لَهُ حَتَّى تَرَوْا أَنَّكُمْ قَد كَافَأْتُمُوهُ )) . حديث صحيح رواه أبو داود والنسائي بأسانيد الصحيحين .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kutaka ulinzi kwa Allaah atapatiwa, na mwenye kutaka kitu kwa Allaah, pia atamtekelezea. Na mwenye kukualika itikia mwaliko wake, na mwenye kuwafanyia wema, na mlipeni na mkikosa cha kumlipa basi muombeeni dua mpaka mkinai kuwa mmemlipa kwa wema aliowafanyia." [Hadiyth Swahiyh iliyonukuliwa na Abu Daawuwd na An-Nasaaiy kwa Isnaad zilizo Swahiyh]