092-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kuihusisha Siku ya Ijumaa kwa Funga au Usiku wake kwa Swalaah Miongoni mwa Masiku Mengine

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب كراهة تخصيص يوم الجمعة بصيام أَوْ ليلته بصلاة من بين الليالي

092-Mlango Wa Ukaraha wa Kuihusisha Siku ya Ijumaa kwa Funga au Usiku wake kwa Swalaah Miongoni mwa Masiku Mengine

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لا تَخُصُّوا لَيْلَةَ الجُمُعَةِ بِقِيَامٍ مِنْ بَيْنِ اللَّيَالِي ، وَلاَ تَخُصُّوا يَومَ الجُمُعَةِ بِصِيَامٍ مِنْ بَيْنِ الأَيَّامِ ، إِلاَّ أَنْ يَكُونَ فِي صَومٍ يَصُومُهُ أحَدُكُمْ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msikhusishe usiku wa Ijumaa kwa ajili ya kuswali Swalaah za Sunnah baina ya masiku mengine wala msikhusishe siku ya Ijumaa kwa ajili ya funga baina ya siku nyengine isipokuwa iwe ni funga ambayo hufunga mmoja wenu." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( لاَ يَصُومَنَّ أحَدُكُمْ يَوْمَ الجُمُعَةِ إِلاَّ يَوماً قَبْلَهُ أَوْ بَعْدَهُ )) . متفق عَلَيْهِ .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Asifunge mmoja wenu siku ya Ijumaa isipokuwa siku kabla yake au baada yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن محمد بن عَبَّادٍ ، قَالَ : سَأَلْتُ جَابِراً رضي الله عنه : أنَهَى النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عَنْ صَومِ الجُمُعَةِ ؟ قَالَ : نَعَمْ . متفق عَلَيْهِ .

Amesema Muhammad bin 'Abbaad: Nilimuuliza Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Hivi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kufunga siku ya Ijumaa?" Akamjibu: "Ndiyo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أُمِّ المُؤمِنِينَ جويرية بنت الحارث رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم دَخَلَ عَلَيْهَا يَوْمَ الجُمُعَةِ وهِيَ صَائِمَةٌ ، فَقَالَ : (( أصُمْتِ أمْسِ ؟ )) قالت : لا ، قَال: (( تُرِيدِينَ أنْ تَصُومِي غَداً ؟ )) قالتْ : لاَ . قَالَ : (( فَأَفْطِرِي )) . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Mama wa Waumini, Juwayriyah bint Al-Haarith (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtembelea siku ya Ijumaa akiwa amefunga, akamuuliza: "Je, ulifunga jana?" Akasema: "Hapana." Akauliza tena: "Je, una niya ya kufunga kesho?" Akasema: "Hapana." Akamwambia: "Fungua (yaani usiendelee kufunga siku ya leo)." [Al-Bukhaariy]

 

 

Share