108-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ukaraha wa Kutoka katika Mji Ambao Umekumbwa na Ugonjwa wa Kuambukiza na Kuingia Ndani yake (Haifai Kuingia Wala Kutoka katika Mji Huo)
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة الخروج من بلد وقع فيها الوباء
فراراً منه وكراهة القدوم عليه
108-Mlango Wa Ukaraha wa Kutoka katika Mji Ambao Umekumbwa na Ugonjwa wa Kuambukiza na Kuingia Ndani yake (Haifai Kuingia Wala Kutoka katika Mji Huo)
قال الله تَعَالَى :
أَيْنَمَا تَكُونُوا يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ ۗ ﴿٧٨﴾
Popote mtakapokuwa yatakufikieni mauti, japo mkiwa katika minara (au ngome) imara na madhubuti. [An-Nisaa: 78]
وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ ﴿١٩٥﴾
Wala msijitupe katika maangamizi [Al-Baqarah: 195]
Hadiyth – 1
وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ عمرَ بن الخطاب رضي الله عنه خرج إلى الشَّامِ حَتَّى إذا كَانَ بسَرْغَ لَقِيَهُ أُمَرَاءُ الأَجْنَادِ - أَبُو عُبَيْدَةَ بنُ الجَرَّاحِ وأصْحَابُهُ - فَأخْبَرُوهُ أنَّ الوَبَاءَ قَدْ وَقَعَ بِالشَّامِ . قَال ابن عباس : فقال لي عمر : ادْعُ لِي المُهَاجِرِينَ الأَوَّلِينَ ، فَدَعَوْتُهُمْ فَاسْتَشَارَهُمْ وَأخْبَرَهُمْ أنَّ الوَبَاءَ قَدْ وَقَعَ بالشَّامِ ، فَاخْتَلَفُوا ، فَقَالَ بَعْضُهُمْ : خَرَجْتَ لأَمْرٍ ، وَلاَ نَرَى أنْ تَرْجِعَ عَنْهُ . وَقَالَ بَعضهم : مَعَكَ بَقِيَّةُ النَّاسِ وأصْحَابُ رسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وَلاَ نَرَى أنْ تُقْدِمَهُمْ عَلَى هَذَا الوَبَاء . فقال : ارْتَفِعُوا عَنِّي . ثُمَّ قَالَ : ادْعُ لِي الأَنْصَارَ ، فَدَعَوْتُهُمْ ، فَاسْتَشَارَهُمْ ، فَسَلَكُوا سَبيلَ المُهَاجِرينَ ، وَاخْتَلَفُوا كاخْتِلاَفِهِمْ ، فقال : ارْتَفِعُوا عَنِّي . ثُمَّ قَالَ : ادْعُ لِي مَنْ كَانَ هاهُنَا مِنْ مَشْيَخَةِ قُريشٍ مِنْ مُهَاجِرَةِ الفَتْحِ ، فَدَعَوْتُهُمْ ، فَلَمْ يَخْتَلِفْ عَلَيْهِ مِنْهُمْ رَجُلاَنِ ، فَقَالُوا : نَرَى أنْ تَرْجِعَ بِالنَّاسِ ، وَلاَ تُقْدِمَهُمْ عَلَى هَذَا الوَبَاءِ ، فَنَادَى عُمَرُ رضي الله عنه في النَّاسِ : إنِّي مُصَبحٌ عَلَى ظَهْرٍ ، فَأَصْبِحُوا عليْهِ ، فقال أبو عبيدة بن الجراح رضي الله عنه : أفِراراً مِنْ قَدَرِ الله ؟ فقالَ عُمرُ رضي الله عنه : لو غَيْرُكَ قَالَهَا يا أبا عبيدَةَ ! – وَكَانَ عُمَرُ يَكْرَهُ خِلاَفَهُ – نَعَمْ ، نَفِرُّ مِنْ قَدَرِ اللهِ إلى قَدَرِ اللهِ ، أرَأيْتَ لَو كَانَ لَكَ إبِلٌ ، فَهَبَطَتْ وَادِياً لَهُ عُدْوَتَانِ ، إحْدَاهُمَا خَصْبَةٌ ، وَالأُخْرَى جَدْبَةٌ ، أَلَيسَ إنْ رَعَيْتَ الخصْبَةَ رَعَيْتَهَا بِقَدَرِ اللهِ ، وَإنْ رَعَيْتَ الجَدْبَةَ رَعَيْتَهَا بِقَدَرِ اللهِ ؟ قَالَ : فَجَاءَ عَبدُ الرَّحمانِ بنُ عَوفٍ رضي الله عنه ، وَكَانَ مُتَغَيِّباً في بَعْضِ حاجَتِهِ ، فقالَ : إنَّ عِنْدِي من هَذَا علماً ، سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يقولُ : (( إِذَا سَمِعْتُمْ بِهِ بأرْضٍ فَلاَ تَقْدِمُوا عَلَيْهِ ، وَإِذَا وَقَعَ بِأرْضٍ وَأنْتُمْ بِهَا فَلاَ تَخْرُجُوا فِراراً مِنْهُ )) فحمِدَ اللهَ تَعَالَى عمرُ رضي الله عنه وانصَرَفَ . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu), alitoka kwenda Shaam, alipofika Sargha, 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikutana na Kamanda wa Jeshi la Kiislamu - Abu 'Ubayda 'Aamir bin Al-Jarrah akiwa na wenzake, nao wakamueleza kuwa tauni iko katika ardhi ya Shaam. Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: 'Umar akasema: "Niitie Muhaajirun wa mwanzo." Nikawaita na akawataka ushauri na akawaeleza kuwa tauni iko Shaam, wakatofautiana katika rai zao. Baadhi yao wakasema: "Tumetoka kwa jambo ili tulifanikishe, hatuoni sababu kwa nini tuache kulifanikisha", na baadhi yao wakasema: "Unao watu pamoja nawe na wengine ni Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hatuoni sababu ya wewe kuwapeleka katika tauni hii." 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: "Sasa hivi niacheni na nendeni mukaniitie Answaar." Nikaenda kuwaita, akawataka ushauri, na wakaipita njia ya Muhaajirun, na wakakhitilafiana kama walivyo khitilafiana wao (Muhaajirun). 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: "Nendeni ." Kisha akasema: "Niitie wazee wa Kiquraysh wa hapa katika waliohama mwaka wa kufunguliwa Makkah." Nikawaita, nao hawakukhitilafiana, walisema: "Tunaona urudi na hao watu na usiwapeleke kwenye tauni." "Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akatoa wito (tangazo) kwa watu huku akisema: "Mimi asubuhi nitaamka safari (ya kurudi) kwa hiyo nanyi fanyeni safari." Abu 'Ubaydah bin Al-Jarraah (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: "Unaukimbia Uwezo (Qadar) wa Allaah?" 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: "Hayo angali yasema mwengine (lakini si wewe) Abu 'Ubaydah! Kisha 'Umar akajibu: "Ndiyo, tunakimbia Qadar ya Allaah kwa kukimbilia kwenye Qadar ya Allaah, uanonaje kama ungalikuwa na ngamia wakawa katika jangwa lina pande mbili, moja ina rutubu na nyengine kama hivi, je, huoni kuwa utawalisha katika sehemu ya rutuba, utakuwa umewalisha kwa Uwezo (Qadar) wa Allaah na kama ungewalisha kwa Qadar ya Allaah?" Akasema: Muda huo huo akawa ametokea 'Abdur-Rahmaan bin 'Awf (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye hakuwepo kwenda alikwenda kutafuta baadhi ya mahitaji yake akasema: "Katika hili mimi nina ujuzi. Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: 'Kama mtasikia (hiyo tauni) iko kwenye ardhi fulani msiende huko, na kama itakuwa katika ardhi, nanyi mko hapo msitoke kuikimbia." Baada ya maneno hayo 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akamshukuru Allaah, kisha akaondoka (kurudi Madiynah). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أسامة بن زيد رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا سَمِعْتُمُ الطَّاعُونَ بِأَرْضٍ ، فَلاَ تَدْخُلُوهَا ، وَإِذَا وَقَعَ بِأرْضٍ ، وأنْتُمْ فِيهَا ، فَلاَ تَخْرُجُوا مِنْهَا )) . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Usamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mnaposikia kuwa tauni iko kwenye ardhi fulani msiingie humo, na kama itakuwa katika ardhi, nanyi mko hapo msitoke kuikimbia." [Al-Bukhaariy na Muslim]