011-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Nguo Yenye Msalaba
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
011- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Nguo Yenye Msalaba:
Toka kwa ‘Aaishah:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمْ يَكُنْ يَتْرُكُ فِي بَيْتِهِ شَيْئًا فِيهِ تَصَالِيبُ إِلَّا نَقَضَهُ"
“Kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa akiacha chochote ndani ya nyumba yake chenye umbo (au mchoro) la msalaba ila hukiharibu”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5952].