012-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Nguo Iliyotengenezwa Kwa Ngozi Ya Wanyama Wakali
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
012- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Nguo Iliyotengenezwa Kwa Ngozi Ya Wanyama Wakali:
Ni kama simba, chui, duma na kadhalika. Ni haramu kuvaa nguo au viatu vilivyotengenezwa kwa ngozi za wanyama hawa kutokana na neno lake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"لَا تَرْكَبُوا الْخَزَّ وَلَا النِّمَارَ"
“Msikalie hariri wala ngozi ya chui”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4129) na Ibn Maajah (3656)].
Rasuli amekataza kutumia vitu hivi kutokana na kuwa ni mapambo, na kuwa vinajenga kiburi kwa mtumiaji, lakini pia ni nguo za watu wasio na asili ya Uarabu (Waajemi). [‘Awnul Ma’abuwd (11/188)]