10-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Inaruhusiwa Mwanamke Kumsalimia Mwanaume Na Kinyume Chake Lakini Bila Kupeana Mikono
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
أَحْكَامُ النَّظَرِ
Hukumu Za Kuangalia
10-Inaruhusiwa Mwanamke Kumsalimia Mwanaume Na Kinyume Chake Lakini Bila Kupeana Mikono:
Ummu Haani:
"ذَهَبْتُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَامَ الْفَتْحِ فَوَجَدْتُهُ يَغْتَسِلُ، وَفَاطِمَةُ ابْنَتُهُ تَسْتُرُهُ فَسَلَّمْتُ عَلَيْهِ"
“Nilikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwaka ule Makkah ilipokombolewa. Nikamkuta anaoga na binti yake Faatwimah amemwekea pazia, nikamsalimia”. [Al-Bukhaariy (3171) na Muslim (336)].
Hadiyth inatufunza kwamba mwanamke anaweza kumsalimia mwanaume bila kupeana mkono, lakini kama mazingira ya fitnah hayapo.
Na pia mwanaume anaruhusiwa kumsalimia mwanamke bila kupeana mkono. Asmaa bint Yaziyd amesema:
" أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرَّ فِي المَسْجِدِ يومًا، وعُصْبَةٌ منَ النِّسَاءِ قُعُوْدٌ، فَأَلْوَى بِيَدِهِ بالتسليم"
“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipita siku moja Msikitini na kundi la wanawake likiwa limekaa humo. Akawasalimia na kuwaashiria kwa mkono wake”. [At-Tirmidhiy (2697), Abu Daawuwd (5204), Ibn Maajah (3701)].