12-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Kuzungumza Na Mwanaume Kwa Simu Kwa Haja

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

 

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com 

 

12-Kuzungumza Na Mwanaume Kwa Simu Kwa Haja:

 

Mwanamke anaruhusiwa kuzungumza na mwanaume ajinabi kwa simu ya kawaida, mobile na kadhalika kutokana na haja, lakini hilo ni lazima lifungamanishwe na vidhibiti vya kisharia.  Ama ikiwa simu hiyo itaibua kati yao mazingira yanayofanana na hali ya wao kuwa wawili peke yao ambayo inaweza kuwapeleka kwenye mazungumzo yatakayowakokota kwenye uchafu wa zinaa, basi kuacha hilo ni lazima.  Na hii ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam: 

 

"لَا يَخْلُوَنَّ رَجُلٌ بِامْرَأَةٍ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ ثَالثُهُمَا"

 

“Kamwe asibaki mwanaume pweke na mwanamke, kwani shaytwan atakuwa ni wa tatu wao”.  [Ahmad katika Al-Musnad (1/18) kwa Sanad Swahiyh]

 

 

 

Share