01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: Mambo Mawili Muhimu Kuyajua

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ 

 

Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo

 

 

الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ

 

Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu

  

Alhidaaya.com 

 

 

001-Mambo Mawili Muhimu Kuyajua:

 

Imeshaelezwa nyuma kwamba mwanamke haruhusiwi kuonyesha pambo lake isipokuwa kwa mumewe, au maharimu zake, au wanawake wenzake na wengineo wote waliotajwa.  Katika suala hili, yamebakia mambo mawili ambayo ni lazima yajulikane:

                                                                 

La kwanza:  Ni kwamba pambo ambalo mwanamke analionyesha kwa watajwa hawa linatofautiana na kuzidiana.  Pambo analolionyesha kwa mumewe si sawa na analolionyesha kwa baba yake au kaka yake, na analolionyesha kwa baba yake na kaka yake si sawa na analolionyesha kwa mume wa baba yake na kuendelea.  Jambo hili bila shaka liko wazi.

 

La pili:  Kujipamba kwake kwa mumewe kuna mipaka, hakuachiwa ajipambe tu.  Kwa mfano, haruhusiwi kujipamba kwa kitu kilichoharamishwa, au cha kujifananisha na wanaume, au chenye kugeuza uumbaji wa Allaah, au kilicho maalum kwa mapambo ya wanawake wa kikafiri na vitakavyobainika katika yanayokuja.

 

 

 

Share