02-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: Aina Za Mapambo Ambayo Mwanamke Anajipambia

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ

 

Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo

 

 

الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ

 

Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu

  

Alhidaaya.com 

 

 

02-Aina Za Mapambo Ambayo Mwanamke Anajipambia

 

1-Pambo La Nywele:

 

Inapendeza kwa mwanamke kuzitunza vyema nywele zake kwa kuzichana, kuzitia mafuta, kuziosha na mfano wa hivyo ili aonekane mbele ya mumewe kwa mandhari inayomfurahisha.  Na bila shaka kumfurahisha mume ni jambo linalotakiwa kisharia.  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipoulizwa kuhusu mwanamke bora kabisa alijibu: 

 

"الَّتِي تُطِيعُهُ إِذَا أَمَرَ، وتَسُرُّهُ إِذَا نَظَرَ، وَتَحْفَظُهُ فِي نَفْسِهَا وَمَالِهِ"

 

“Ni yule ambaye anamsikiliza anapomwamrisha, anamfurahisha anapomwangalia, na anamlinda kwa kuuhifadhi mwili wake (na machafu) na mali yake.  [An-Nasaaiy: (6/68) kwa Sanad Swahiyh].

 

Na kwa sababu hii, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anawakataza Maswahaba wake wanaporudi kutoka safari kuingia nyumbani kwa wake zao usiku kwa kuchelea mtu kumkuta mkewe katika mandhari isiyoridhisha.  Alikuwa akisema:

 

"أَمْهِلُوا حَتَّى لا نَدْخُلَ لَيْلاً ، كَىْ تَمْتَشِطَ الشَّعِثَةُ وَتَسْتَحِدَّ الْمُغِيبَةُ ‏"

 

“Vuteni muda tusipate kuingia (majumbani) usiku, ili mwenye nywele zilizokaa ovyo ovyo apate muda wa kuzitengeneza, na anyoe kinena ambaye mumewe amekuwa mbali naye”.  [Al-Bukhaariy (579) na Muslim (715)]

 

Na Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasema:

 

"مَنْ كَانَ لَهُ شَعْرٌ فَلْيُكْرِمْهُ"

 

“Mwenye nywele, basi azienzi na kuzitunza”.  [Abu Daawuwd (4163) kwa Sanad Hasan].

 

Miongoni Mwa Adabu Za Kuchana Nywele:

 

1-  Kuanza upande wa kulia wa kichwa

 

Ni kwa Hadiyth ya ‘Aaishah:

 

 "كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  يُحِبُّ التَّيَمُّنَ مَا اسْتَطَاعَ فِي طُهُورِهِ وَتَنَعُّلِهِ وَتَرَجُّلِهِ" 

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapenda kuanzia kulia kiasi awezavyo wakati anapojitwaharisha, anapovaa viatu na anapochana nywele zake”.  [Sunan An-Nasaai (26)]

 

2-  Kuzitia mafuta na kuzilainisha kwa maji kama zimetutumka

 

Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati alipomwona mtu mwenye nywele zilizosimama vibaya:

 

 "أَمَا يَجِدُ هَذَا مَا يُسَكِّنُ بِهِ شَعْرَهُ ‏"‏ ‏

 

 “Je, hawezi kupata huyu chochote akazilainisha nywele zake?!   [Abu Daawuwd (4062) na An-Nasaaiy (8/183) kwa Sanad Swahiyh]

 

 

 

 

Share