09-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: Mwanamke Ampake Mumewe Mafuta

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ 

Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo

 

 

الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ

Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

09-Mwanamke Ampake Mumewe Mafuta:

 

‘Aaishah:   

 

"كُنْتُ أُطَيِّبُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ   بِأَطْيَبِ مَا نَجِدُ حَتَّى أَجِدَ وَبِيصَ الطِّيبِ فِي رَأْسِهِ وَلِحْيَتِهِ"

 

“Nilikuwa nampaka Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mafuta mazuri zaidi tuliyonayo mpaka naona mng’ao wa mafuta kwenye kichwa chake na ndevu zake”.  [Al-Bukhaariy (5923) na Muslim (1190)]

 

Katika Hadiyth hii, tutagundua kwamba wanaume hawapaki au kupakwa na wake zao mafuta usoni kinyume na wanawake, wao ndio maumbile yao ya kujipodoa uso na kujipamba kwa mafuta mazuri na vinginevyo kinyume na wanaume, wao kufanya hayo ni marufuku ili wasijifananishe na wanawake.  [Fat-hul Baariy (10/366)]

 

 

Share