10-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: Mwanamke Akitoka Nyumbani Kwake Kwenda Nje Ni Lazima Aondoshe Harufu Ya Mafuta Mazuri

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ 

Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo

 

 

الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ

Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

10-Mwanamke Akitoka Nyumbani Kwake Kwenda Nje Ni Lazima Aondoshe Harufu Ya Mafuta Mazuri:

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"أَيُّما امرَأَةٍ اسْتَعْطَرَتْ فَمَرَّتْ بِقَوْمٍ لِيَجِدُوا رِيْحَهَا فَهِيَ زَانِيَةٌ"

 

“Mwanamke yeyote aliyejitia mafuta mazuri kisha akajipitisha kwa wanaume ili waisikie harufu yake, basi anakuwa ni mwenye kuzini”.  [Takhriyj yake imetajwa nyuma]

 

Na anasema tena Rasuli:

 

"إِذَا شَهِدَتْ إِحْدَاكُنَّ الْمَسْجِدَ فَلَا تمَسَّ طِيْبًا"

 

“Akihudhuria mmoja wenu masjid, basi asiguse mafuta mazuri”.    [Muslim (334) na An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (9425)]   

 

Sheikh Al-Albaaniy (Rahimahul Laah) amesema:  “Ikiwa hili ni haramu kwa mwanamke anayekwenda masjid, basi vipi itakuwa hali kwa mwenye kwenda sokoni, au kupita vichochoroni na mabarabarani?!  Bila shaka itakuwa ni haramu zaidi na madhambi makubwa zaidi”. 

 

Al-Haythamiy ameeleza katika “Az-Zawaajir” kwamba mwanamke kutoka nyumbani kwake akiwa amejipamba na kujitia mafuta mazuri, ni katika madhambi makubwa hata kama mumewe atamruhusu.

 

Ninasema:  “Ni lazima mwanamke amalizane na harufu za manukato kabla hajatoka nyumbani kwake kwa njia yoyote awezayo kama kuosha na kadhalika”.

 

Angalizo:

 

Mwanamke anaweza kutoka nyumbani kwake bila kuwa amejitia manukato lakini akawa amembeba mwanaye ambaye amemtia manukato.  Hili halifai, kwa kuwa sababu ya kuvuta macho ya wanaume kwake kutokana na harufu nzuri itakuwa bado iko, na hivyo basi hukmu ya kuwa ni haramu inabakia palepale.  Atanabahi kwa hili, na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.

 

 

Share