11-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: Hairuhusiwi Kutumia Mafuta Mazuri, Si Kwa Mume Wala Kwa Mwengine Yeyote Katika Hali Tatu
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo
الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ
Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu
11-Hairuhusiwi Kutumia Mafuta Mazuri, Si Kwa Mume Wala Kwa Mwengine Yeyote Katika Hali Tatu:
Ya kwanza: Baada ya kuhirimia Hajji au ‘Umrah:
Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na aliyehirimia Hajji au ‘Umrah:
"وَلاَ تَلْبَسُوا مِنَ الثِّيَابِ شَيْئًا مَسَّهُ الزَّعْفَرَانُ وَلاَ الْوَرْسُ"
“Wala msivae nguo yoyote iliyoingiwa na zafarani wala wars”…. [Al-Bukhaariy. Takhriyj yake iko kwenye mlango wa Hijja]
Hikma ya kuzuiwa mwanamke aliyehirimia, ni kuwa harufu ya mafuta haya ni katika vichangamshi na vichochezi vya jimai ambayo inaharibu ihraam.
Ya pili: Katika eda
Mwanamke anakatazwa kutumia mafuta mazuri wakati wa eda ya kufiwa na mumewe.
Ya tatu: Anapotoka nyumbani
Na hii ni hata kama atamkusudia mumewe kama tulivyotangulia kugusia hili nyuma kidogo.