035-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Hukumu Ya Mwenye Kukubali Halafu Akaacha kwa Uvivu Au Kuibadili?

 

200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

035-Ni Ipi Hukumu Ya Mwenye Kukubali Halafu Akaacha kwa Uvivu Au Kuibadili?

 

 

Swali:

س: ما حكم من أقر بها ثم تركها لنوع تكاسل أو تأويل 

Ni ipi hukumu ya mwenye kukubali halafu akaacha kwa uvivu au kuibadili?

 

Jibu:

 

ج: أما الصلاة  فمن أخرها عن وقتها بهذه الصفة فإنه يستتاب فإن تاب وإلا قتل حدا لقوله تعالى :(فان تابوا وأقاموا الصلاة وآتوا الزكاة فخلوا سبيلهم)  وحديث (أمرت أن أقاتل الناس)  الحديث وغيرها

 أما الزكاة  فإن كان مانعها ممن لا شوكة له أخذها الإمام منه قهرا ,ونكله بأخذ شيء من ماله لقوله صلى الله عليه وسلم:( ومن منعها فإنا آخذوها وشطر ماله معها ) الحديث ,وإن كانوا جماعة ولهم شوكة وجب على الإمام قتالهم حتى يؤدوها للآيات والأحاديث السابقة وغيرها وفعله أبو بكر والصحابة رضي الله عنهم أجمعين.

أما الصوم  فلم يرد فيه شيء ولكن يؤدبه الإمام أو نائبه بما يكون زاجرا له ولأمثاله .

أما الحج  فكل عمر العبد وقت له لا يفوت إلا بالموت والواجب فيه المبادرة ,وقد جاء الوعيد الأخروي في التهاون فيه, ولم ترد فيه عقوبة خاصة في الدنيا. 

 

Ama swalaah kuichelewesha nje ya wakati wake kwa sifa yake, atatakiwa kutubia, na kama hataki atauwawa kwa kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ ﴿٥﴾

Lakini wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi waachieni huru njia zao.[At-Tawbah: (9:5)].

 

Na kauli yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

(أمرت أن أقاتل الناس)

"Nimeamrishwa kupigana na watu mpaka washuhudie Allaah” [Al-Bukhaariy, Muslim, Tirmidhiy, Nasaai na Ibn Majah].

 

Na ama Zakaah, ikiwa mtu atajizuia kutoa na hana silaha, Imam atamlazimisha kutoa Zakaah, na kumuadabisha kwa kuchukua chochote kutokana na mali yake hiyo, kwa kauli ya  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

"Na mwenye kujizuia kutotoa Zakaah, basi mimi nitaichukua kwa nguvu, na kuchukua sehemu ya mali yake kama faini”. [Imepokewa na Ahmad 5/2,3, Abu Dawuwd 1575, An-Nasaai 2515, Ibn Abi Shaybah 1613, AbduRazzaq 1814, Al-Baihaqi 4/105, Al-Hakim 1/398].

 

Wakiwa wengi na wana silaha ni wajibu wa Imam  kupambana nao mpaka walipe Zakaah, kwa mujibu wa Aayah  na Hadiyth tulizotangulia kuzitaja na nyinginezo. Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) na Swahaaba wengine walifanya hivyo. Ama kuhusu swawm hakuna dalili iliyopokelewa kuelezea, ila ataadabishwa na Imam au Naibu wake, kwa kumkemea na mfano wake, ama Hijjah ni kwa kila umri wa mtu alioupanga kuhiji, na haupiti mpaka afe tu. Ila inamlazimu kuhiji haraka na kuna kemeo kali la Aakherah kuhusiana na kuzembea kwake, japo duniani hakuna adhabu maalumu iliyotajwa.

 

 

Share