036-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Maana Ya Iymaan?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
036-Nini Maana Ya Iymaan?
Swali:
س: ماهو الإيمان
Ni ipi Iymaan?
Jibu:
ج: الإيمان قول وعمل قول القلب واللسان وعمل القلب واللسان والجوارح ويزيد بالطاعة وينقص بالمعصية ويتفاضل أهله فيه.
Iymaan ni kauli na matendo, kauli ya moyo na ulimi na ni tendo la moyo, ulimi pamoja na viungo, na Iymaan inaongezeka kwa ucha-Mungu na kupungua kwa maasi na watu huzidiana kwa Iymaan zao.