037-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Kauli na Matendo?

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

037-Ni Ipi Dalili Ya Kauli na Matendo?

 

 

Swali:

 

س: ما الدليل على كونه قولا وعملا

Ni ipi dalili ya kauli na matendo?

 

Jibu:

 

ج: قال الله تعالى( ولكن الله حبب إليكم الإيمان وزينه في قلوبكم )الآية وقال تعالى( فآمنوا بالله ورسوله )وهذا معنى الشهادتين اللتين لا يدخل العبد في الدين إلا بهما, وهي من عمل القلب اعتقادا ,ومن عمل اللسان نطقا لا تنفع إلا بتواطئهما وقال تعالى( وما كان الله ليضيع إيمانكم )يعني صلاتكم إلى بيت المقدس قبل تحويل القبلة, سمى الصلاة كلها إيمانا وهي جامعة لعمل القلب واللسان والجوارح.

وجعل النبي صلى الله عليه وسلم الجهاد وقيام ليلة القدر وصيام رمضان وقيامه وأداء الخمس وغيرها من الإيمان, وسئل النبي صلى الله عليه وسلم: أي الأعمال أفضل؟ قال( إيمان بالله ورسوله ).

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amesema:

 

وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ حَبَّبَ إِلَيْكُمُ الْإِيمَانَ وَزَيَّنَهُ فِي قُلُوبِكُمْ َ﴿٧﴾

Lakini Allaah Amekupendezesheeni Iymaan, na Akaipamba katika nyoyo zenu [Al-Hujuraat: (49:7)]

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ  ﴿١٥٨﴾

Basi mwaminini Allaah na Rasuli Wake; [Al-A'raaf: (7:157)]

 

Hii ndio maana ya shahaadah mbili ambazo mja hawezi kuingia katika dini isipokuwa kwa hizo nayo ni amali ya moyo kuitakidi na amali ya ulimi ni kutamka. Na hazinufaishi mpaka ziwe zimetulia katika moyo na ulimi.

 

Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ  ﴿١٤٣﴾

Na Allaah Hakuwa Mwenye Kupoteza Iymaan yenu. [Al-Baqarah: (2:143)]

 

Kwa maana ya kwamba Allaah hawezi kupoteza Swaalah zenu mlizokuwa mkielekea Baytil-Maqdis (Jerusalem) kabla ya kugeuzwa qibla na kuwa Makkah. Swaalah yote imeitwa ni Iymaan, nayo inakusanya matendo ya moyo, ulimi na viungo.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaifanya Jihaad, kisimamo cha Laylatul-Qadri, kufunga Swawm ya Ramadhwaan na kisimamo chake, kuswali Swaalah tano na nyinginezo ni katika Iymaan. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa hivi: Ni matendo gani bora zaidi? Nabiy akajibu ni: "Kumuamini Allaah na Rasuli Wake". [Imepokewa na Al-Bukhaariy (26) na Muslim (83) katika Hadiyth ya Abu Huraiyrah]

 

 

Share