20-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Wanawake Walioharamika Kwa Muda: v-Mpagani Mpaka Asilimu

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

  

Alhidaaya.com 

 

 

20-Wanawake Walioharamika Kwa Muda:  5-Mpagani Mpaka Asilimu:

 

Ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:

 

 "وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ"

 

“Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini.  Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni”.  [Al-Baqarah: 221]

 

Na Amesema tena Allaah Ta’aalaa:

 

  "وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ"

 

“Na wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa”.  [Al-Mumtahinah: 10]

 

Ndani ya aayah hizi mbili, kuna katazo la kuoa wanawake makafiri mpaka wasilimu.  Katika Hadiyth ya Al Mis-war bin Al-Makhramah -kuhusiana na Suluhu ya Al-Hudaybiyah-, ni kwamba iliposhuka Kauli Yake Ta’aalaa: 

 

  "وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ"

 

“Na wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa. 

 

‘Umar aliwataliki wake zake wawili  wakati huo ambao alikuwa nao wakati wa ushirikina, na Mu’aawiyah bin Abiy Sufyaan akamwoa mmoja wao, na mwingine akaolewa na Swafwaan bin ‘Umayyah”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2734)]  

 

 

Share