19-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Wanawake Walioharamika Kwa Muda: iv-Aliyeachwa Talaka Tatu

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

  

Alhidaaya.com 

 

 

19-Wanawake Walioharamika Kwa Muda: 4-Aliyeachwa Talaka Tatu:

 

Mwanamke huyu hawezi kuwa halali tena kwa mumewe ila baada ya kuolewa na mume mwingine ndoa sahihi.  Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:

 

" فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ مِن بَعْدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ ۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يَتَرَاجَعَا إِن ظَنَّا أَن يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۗ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ"

 

“Na akimtaliki (mara ya tatu), basi hatokuwa halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwengine.  Akimtaliki (au akifariki) hapatokuwa dhambi juu yao wawili kurejeana wakidhani kwamba watasimamisha Mipaka ya Allaah.  Na hiyo ni Mipaka ya Allaah Anaibainisha kwa watu wanaojua”.  [Al-Baqarah: 230]

 

Hili litakuja kufafanuliwa kwa mapana zaidi katika hukumu za talaka In Shaa Allaah.

 

 

Share