24-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Haijuzu Kumwoa Mwanamke Mzinifu (Kahaba) Ila Kwa Masharti Mawili

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

  

Alhidaaya.com 

 

 

 

 

24-Haijuzu Kumwoa Mwanamke Mzinifu (Kahaba) Ila Kwa Masharti Mawili:

 

La kwanza: 

 

Atubie kikweli na aachane na tabia hiyo.  Kwa kuwa, kama atatubia, atakuwa ameondokewa na sifa ambayo ilikuwa ni sababu ya kuharamishwa kumwoa kwa mujibu wa aayah tukufu.   Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"التَّائِبُ مِنَ الذَّنْبِ كَمَنْ لَا ذَنْبَ لَهُ"

 

“Aliyetubia dhambi ni kama ambaye hakutenda dhambi”.  [Al-Albaaniy ameihasanisha. Imekharijiwa na Ibn Maajah (4250), Ibn Al-Ja’ad (1/266), Al-Qadhwaaiy katika “Ash-Shihaab” (1/97), na At-Twabaraaniy (10/150)]

 

Ya pili: 

 

Asiwe na chochote tumboni, na hili litathibitishwa kwa kupata hedhi moja.  Hili ni sharti kwa Ahmad na Maalik kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na wanawake waliotekwa vitani:

 

"لاَ تُوطَأُ حَامِلٌ حَتَّى تَضَعَ وَلاَ غَيْرُ ذَاتِ حَمْلٍ حَتَّى تَحِيضَ حَيْضَةً"

 

“Mjamzito haingiliwi mpaka ajifungue, na asiye mjamzito mpaka apate hedhi moja”.  [Hasanun Bitwuruqihi.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2157) na Ahmad (3/62)]

 

Kijakazi au mwanamke aliyetekwa vitani, ni lazima ihakikishwe kwamba hana kitu tumboni kabla hajaingiliwa, na mwanamke mzinifu pia kabla hajaolewa.  Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.

 

 

Share