25-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Wanawake Walioharamika Kwa Muda: vii-Mwanamke Aliyehirimia Mpaka Afunguke Na Ihraam
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الزَّوَاجِ
Kitabu Cha Ndoa
25-Wanawake Walioharamika Kwa Muda: vii-Mwanamke Aliyehirimia Mpaka Afunguke Na Ihraam:
Si halali kwa mwanaume au mwanamke aliyehirimia Hajji kufunga ndoa wakiwa katika ihraam. Yeyote kati yao akifunga ndoa, basi ndoa ni batili. Haya ni madhehebu ya Jumhuwr. Ni kutokana na Hadiyth ya ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"لا يَنْكِحُ اَلْمُحْرِمُ، وَلَا يُنْكحُ، وَلَا يَخْطُبُ"
“Aliyehirimia haoi, wala haozeshwi, wala hachumbii”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (1409), At-Tirmidhiy (840), Abu Daawuwd (1841), An-Nasaaiy (5/292) na Ibn Maajah (1966)]