040-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Inayojulisha Iymaan inakusanya Mfumo Mzima Wa Dini?

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

 

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

040-Ni Ipi Dalili Inayojulisha Iymaan inakusanya Mfumo Mzima Wa Dini?

 

 

Swali:

 

س: ما الدليل على أن الإيمان يشمل الدين كله عند الإطلاق

 

Ni ipi dalili inayojulisha Iymaan inakusanya mfumo mzima wa dini?

 

Jibu:

 

ج: قال النبي صلى الله عليه وسلم في حديث وفد عبد القيس:( آمركم بالإيمان بالله وحده قال أتدرون ما الإيمان بالله وحده؟ قالوا الله ورسوله أعلم. قال: شهادة أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله ,وإقام الصلاة ,وإيتاء الزكاة ,وأن تؤدوا من المغنم الخمس ).

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema katika Hadiyth ya ujumbe wa ‘Abdul-Qais: "Ninakuamrisheni kumuamini Allaah Pekee.”

Akawauliza! Je, mnajua nini maana ya kumuamini Allaah Pekee? Wakamjibu: “Allaah na Rasuli Wake ndio Wajuzi zaidi”.

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema:

 

"Ni kutoa Shahaadah mbili, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakkah na kutekeleza miongoni mwa ngawira kutoa tano yake" [Imepokewa na Al-Bukhaariy (17) na Muslim (17)].

 

 

Share