041-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Inayojulisha Juu Ya Nguzo Sita Za Iymaan?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
041-Ni Ipi Dalili Inayojulisha Juu Ya Nguzo Sita Za Iymaan?
Swali:
س: ما الدليل على تعريف الإيمان بالأركان الستة عند التفصيل
Ni ipi dalili inayojulisha juu ya nguzo sita za Iymaan?
Jibu:
ج: قول النبي صلى الله عليه وسلم لما قال جبريل عليه السلام أخبرني عن الإيمان قال( أن تؤمن بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر وتؤمن بالقدر خيره وشره )
Ni kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale Jibriyl (‘Alayhi Salaam) alipomwambia nipe habari kuhusiana na Iymaan Nabiy alimtajia kwa kusema:
"Ni Kumuamini Allaah, Malaaikah Wake, Vitabu Vyake, Rasuli Wake, Siku ya Mwisho na kuamini Qadari Yake (Allaah) ya kuwa kheri na shari vinatoka Kwake (Subhaanahu wa Ta'aalaa). [Imepokewa na Muslim-Kitaabul-Iymaan].