046-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Shirki Kubwa?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
046-Ni Ipi Shirki Kubwa?
Swali:
س: ما هوالشرك الأكبر
Ni ipi shirki kubwa?
Jibu:
: هو اتخاذ العبد من دون الله ندا يسويه برب العالمين يحبه كحب الله ويخشاه كخشية الله ويلتجئ إليه ويدعوه ويخافه ويرجوه ويرغب إليه ويتوكل عليه أو يطيعه في معصية الله أو يتبعه على غير مرضاة الله وغير ذلك قال تعالى( إن الله لا يغفر أن يشرك به ويغفر ما دون ذلك لمن يشاء ومن يشرك بالله فقد افترى إثما عظيما )وقال تعالى( ومن يشرك بالله فقد ضل ضلالا بعيدا )وقال تعالى( ومن يشرك بالله فقد حرم الله عليه الجنة ومأواه النار )وقال تعالى( ومن يشرك بالله فكأنما خر من السماء فتخطفه الطير أو تهوي به الريح في مكان سحيق )وغير ذلك من الآيات
وقال النبي صلى الله عليه وسلم( حق الله على العباد أن يعبدوه ولا يشركوا به شيئا وحق العباد على الله أن لا يعذب من لا يشرك به شيئا )وهو في الصحيحين, ويستوي في الخروج بهذا الشرك عن الدين المجاهر به ككفار قريش وغيرهم, والمبطن له كالمنافقين المخادعين الذين يظهرون الإسلام ويبطنون الكفر, قال الله تعالى( إن المنافقين في الدرك الأسفل من النار ولن تجد لهم نصيرا إلا الذين تابوا وأصلحوا واعتصموا بالله وأخلصوا دينهم لله فأولئك مع المؤمنين )وغير ذلك من الآيات.
Ni mtu kumfanya kiumbe sawa na Allaah katika ushirika wa kumuomba kinyume cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala). Anampenda mfano wa kumpenda Allaah, anamuogopa kama anavyomuogopa Allaah, anakimbilia kwake na kumuomba, anamuogopa na kumtegemea, au kumtii katika kumuasi Allaah au kumfuata katika yasiyompendeza Allaah na mengineyo.
Ni kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾
Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa, lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu kabisa. [An-Nisaa: (4:48)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١١٦﴾
Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali. [An-Nisaa: (4:116)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾
Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru. [Al-Maaidah: (5:72)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَانٍ سَحِيقٍ ﴿٣١﴾
Na yeyote anayemshirikisha Allaah, basi ni kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, wakamnyakua ndege au upepo ukamtupa mahali mbali mno. [Al-Hajj: (22:31)]
Na Aayah nyenginezo.
Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Haki ya Allaah kwa waja ni kumuabudu Yeye bila kumshirikisha na kitu chochote na haki ya waja kwa Allaah ni kutomuadhibu yule ambae hamshirikishi Allaah na kitu chochote”.
Hadiyth hiyo ipo katika Swahiyh mbili [Al-Bukhaariy (2856) na Muslim (30)].
Na wanalingana katika shirki hii kutoka katika dini mwenye kujidhihirisha kwayo kama makafiri wakikuraishi na wengineyo, na wenye kuficha ukafiri wao kama wanafiki na kujidhahirisha na Uislamu. Allaah (عزَّ وجلَّ) Anasema:
إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا ﴿١٤٥﴾
Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika moto, na wala hutompata kwa ajili yao mwenye kunusuru.
إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَاعْتَصَمُوا بِاللَّـهِ وَأَخْلَصُوا دِينَهُمْ لِلَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَسَوْفَ يُؤْتِ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٤٦﴾
Isipokuwa wale waliotubu, na wakarekebisha mwenendo wao, na wakashikamana na Allaah, na wakakhalisisha Dini yao kwa ajili ya Allaah, basi hao watakuwa pamoja na Waumini. Na Allaah Atawapa Waumini ujira mkubwa kabisa. [An-Nisaa: (4:145-146)]