01-Malaika: Malaika Ni Nani?

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

 01:  Malaika Ni Nani?

 

 

Malaika ni viumbe kati ya Viumbe vya Allaah Ta’aalaa.  Allaah Amewaumba kutokana na nuru.  Ni viumbe waliopewa hishma kubwa, hawamwasi Allaah kwa Anayowaamuru kuyafanya, wanatekeleza yote wanayoamuriwa, na hawana jinsia ya kiume wala ya kike.  Hawali, hawanywi, hawaoani, hawachoki, hawahisi tabu, na hakuna ajuaye idadi yao isipokuwa Allaah Ta’aalaa.

 

Allaah Ta’aalaa Amewawekea kizuizi tusiweze kuwaona, lakini Anaweza kuwafichulia baadhi ya Waja Wake wakaweza kuwaona, na Malaika hawa wana uwezo wa kujiweka katika maumbo tofauti, na wana nguvu kubwa na uwezo wa hali ya juu kabisa wa kugura kutoka sehemu moja hadi nyingine.

 

Sheikh Ibn ‘Uthaymiyn amesema: “Malaika ni ulimwengu uliofichika kwetu (ghayb), ni viumbe walioumbwa, na wanamwabudu Allaah Ta’aalaa Pekee. Hawana sifa zozote za kimola wala kiungu, na Allaah ‘Azza wa Jalla Amewaumba kutokana na nuru, na Amewapa sifa ya utiifu kamili wa Maamrisho Yake kwao na nguvu ya kuyatekeleza, nao ni wengi mno, na hakuna ajuaye idadi yao isipokuwa Allaah Ta’aalaa”.

 

 

 

Share