21-Malaika: Malaika Wenye Sura Na Maumbo Ya Kutisha: (4)- Malaika Wenye Kutoa Roho Ya Kafiri

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

21:  Malaika Wenye Sura Na Maumbo Ya Kutisha

 

(4)-  Malaika Wenye Kutoa Roho Ya Kafiri

 

Al-Baraa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaah ‘anhu):   “Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuhusiana na kutoka roho:

 

"وإنَّ العَبدَ الكافِرَ إذا كان في انقِطاعٍ مِنَ الدُّنيا وإقبالٍ مِنَ الآخرةِ، نزل إليه من السَّماءِ مَلائِكةٌ سُودُ الوُجوهِ"

 

“Na hakika mja kafiri anapokuwa karibu na kuaga dunia na kuikabili aakhirah, humteremkia kutoka mbinguni Malaika wenye nyuso nyeusi”.  [Hadiyth Swahiyh. Swahiyhul Jaami’i].

 

Wanakuja kwa nyuso hizo kuonyesha hasira yao kwa anayekufa.  Hiyo ndiyo hatima ya makafiri.  Mbali ya kujiwa na nyuso hizo nyeusi, Malaika hao watawapiga nyuso zao na migongo yao katika hali ambayo Rasuli anaambiwa kama angeliona wanavyopigwa, basi angeliona jambo la kutisha mno.  Allaah Ta’aalaa Anasema:

 

"وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ يَتَوَفَّى الَّذِينَ كَفَرُوا ۙ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ"

 

“Na lau ungeliona pale Malaika wanapowafisha wale waliokufuru, wanawapiga nyuso zao na migongo yao na (wanawaambia): Onjeni adhabu iunguzayo”.  [Al-Anfaal: 50]

 

 

Share