31-Malaika: Aina Za Ibada Ambazo Malaika Wanazifanya: (2)- Kupanga Safu Zilizonyooka Kwa Ajili Ya Ibada

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

31:  Aina Za Ibada Ambazo Malaika Wanazifanya

 

(2)- Kupanga Safu Zilizonyooka Kwa Ajili Ya Ibada

 

Allaah Ta’aalaa Anasema Akiizungumzia kauli ya Malaika Wake:

 

"وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ"

 

Na hakika sisi bila shaka ni wenye kujipanga safu safu (kwa ‘ibaadah)”.  [As-Swaaffaat: 165]

 

Malaika hawa hujipanga safu huko mbinguni, safu zilizonyooka barabara, baadhi yao pembeni ya wengine kwa ajili ya kumwabudu Allaah ikiwa ni pamoja na swalah na ibada nyinginezo.

 

 

Toka kwa Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 

 

" أَلاَ تَصُفُّونَ كَمَا تَصُفُّ الْمَلاَئِكَةُ عِنْدَ رَبِّهِمْ؟‏ قَالُوا: وَكَيْفَ تَصُفُّ الْمَلاَئِكَةُ عِنْدَ رَبِّهِمْ؟ قَالَ: ‏ يُتِمُّونَ الصَّفَّ الأَوَّلَ ثُمَّ يَتَرَاصُّونَ فِي الصَّفِّ"

 

“Kwa nini msipange safu kama wanavyopanga safu Malaika kwa Mola wao? Tukasema:  Ee Rasuli wa Allaah, vipi Malaika wanapanga safu kwa Mola wao? Akasema:  Wanakamilisha safu baada ya safu, na wanajipanga vizuri bila kuacha pengo katika safu”.   [Swahiyh Ibn Maajah (818)]

 

Kunyoosha safu kunakuwa ndio ukamilifu na utimilifu wa swalaah kwa Waislamu wanaposwali kama alivyoamuru Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam).  Jambo hili pia ni katika mambo bora tuliyohusishwa nayo sisi Umma wa Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam).  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:

 

"فُضِّلْنَا عَلَى النَّاسِ بِثَلَاثٍ جُعِلَتْ صُفُوفُنَا كَصُفُوفِ الْمَلَائِكَةِ وَجُعِلَتْ لَنَا الْأَرْضُ كلهَا مَسْجِدا وَجعلت تربَتهَا لنا طَهُورًا إِذَا لَمْ نَجِدِ الْمَاء"َ

 

“Tumefanywa bora kuliko umma zilizotangulia kwa mambo matatu:  Safu zetu zimefanywa kama safu za Malaika, na ardhi yote imefanywa kwetu kuwa sehemu ya kuswalia, na mchanga wake umefanywa kitwaharishio chetu tukikosa maji”.  [Muslim (526)]

 

 

Share