39-Malaika: Kazi Za Malaika: (2)- Miykaaiyl (‘alayhis salaam): Anasimamia Mawingu Ya Kuleta Mvua Na Mimea

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

39:   Kazi Za Malaika:

 

(2)- Miykaaiyl (‘alayhis salaam):  Anasimamia Mawingu Ya Kuleta Mvua Na Mimea:

 

‘Ulamaa wengi wameeleza kwamba Malaika aliyepewa jukumu la kuendesha mawingu ya mvua na kuyapeleka pale ambapo Allaah Anamwamuru, ni Miykaaiyl (‘alayhis salaam).  Wamesema hivyo kwa kutegemea Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) aliyesema:

 

"أقبلَتْ يهودُ إلى رَسولِ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم فقالوا: يا أبا القاسِمِ، إنَّا نسألُك عن خمسةِ أشياءَ، فإن أنبَأْتَنا بهِنَّ عرَفْنا أنَّك نبيٌّ واتَّبَعْناك، فأخَذ عليهم ما أخَذ إسرائيلُ على بَنِيه؛ إذ قالوا: اللهُ عَلَى مَا نَقُولُ وَكِيلٌ، قال: هاتوا، قالوا:... ليس من نبيٍّ إلَّا له مَلَكٌ يأتيه بالخبَرِ، فأخبِرْنا مَن صاحِبُك؟ قالجبريلُ عليه السَّلامُ، قالواجِبريلُ! ذاك الذي يَنزِلُ بالحَرْبِ والقِتالِ والعَذابِ، عَدُوُّنا! لو قُلتَميكائيلُ الذي يَنزِلُ بالرَّحمةِ والنَّباتِ والقَطرِ، لكان! فأنزل اللهُ عزَّ وجلَّمَنْ كَانَ عَدُوًّا لِجِبْرِيلَ..."

 

“Mayahudi walikwenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakamwambia:  Ee Abal Qaasim!  Sisi tutakuuliza mambo matano, kama utatujibu, basi tutajua kwamba wewe kweli ni Mtume, na sisi tutakuamini.  Rasuli akachukua kutoka kwao ahadi ile ile ambayo Israaiyl aliichukua toka kwa wanawe, nao wakasema:  Allaah Ni Mdhamini kwa haya tunayoyasema.  Akawaambia:  Yaleteni.  Wakasema:  Hakuna Nabiy yeyote isipokuwa ana Malaika ambaye anamletea habari.  Hebu tueleze, ni nani Malaika wako?  Akasema:  Ni Jibriyl (‘alayhis salaam).  Wakasema:  Huyo ndiye yule anayeteremsha vita, mapigano na adhabu, huyu ni adui yetu.  Lau ungelisema Miykaaiyl ambaye anateremsha rahmah, mimea na mvua, basi lingetimu jambo letu.  Na hapo Allaah Akateremsha:  

 

"قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ"

“Sema:  Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na mwongozo na bishara kwa Waumini”.  [Hadiyth Swahiyh.  Ahmad (2483) na An-Nasaaiy (9072 katika As-Sunan Al-Kubraa.  Ipo pia katika As-Silsilat As-Swahiyhah 4/191]

 

Ibn Al-Qayyim amesema:  “Jibriyl ndiye mwenye dhamana ya kuteremsha wahyi ambao ndio uhai kwa nyoyo na roho, na Miykaaiyl ndiye mwenye dhamana ya mvua ambayo ndio uhai kwa ardhi, mimea na wanyama”.

 

Ibn Baaz naye kasema:  “Miykaaiyl kapewa jukumu la kusimamia maji na mvua”.

 

Na Ibn ‘Uthaymiyn kasema:  “Tunaamini kwamba Malaika wana kazi walizobebeshwa, na kati yao ni Miykaaiyl ambaye anasimamia mvua na mimea”. 

 

 

Share