051-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Tawhiyd Ya Majina Ya Allaah Pamoja Na Sifa Zake?

 

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

 

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

051-Ni Ipi Tawhiyd Ya Majina Ya Allaah Pamoja Na Sifa Zake?

 

 

 

Swali:

س: ما هو توحيد الأسماء والصفات

 

Ni Ipi Tawhiyd Ya Majina Ya Allaah Pamoja Na Sifa Zake?

 

Jibu:

 ج: هو الإيمان بما وصف الله تعالى به نفسه في كتابه ووصفه به رسوله صلى الله عليه وسلم من الأسماء الحسنى والصفات العلى, وإمرارها كما جاءت بلا كيف كما جمع الله تعالى بين إثباتها ,ونفي التكييف عنها في كتابه في غير موضع كقوله تعالى( يعلم ما بين أيديهم وما خلفهم ولا يحيطون به علما )وقوله تعالى( ليس كمثله شيء وهو السميع البصير )وقوله تعالى( لا تدركه الأبصار وهو يدرك الأبصار وهو اللطيف الخبير )وغير ذلك, وفي الترمذي عن أبي بن كعب رضي الله عنه أن المشركين قالوا لرسول الله صلى الله عليه وسلم -يعني لما ذكر آلهتهم- انسب لنا ربك فأنزل الله تعالى( قل هو الله أحد الله الصمد )والصمد الذي( لم يلد ولم يولد )لأنه ليس شيء يولد إلا سيموت وليس شيء يموت إلا سيورث وإن الله تعالى لا يموت ولا يورث( ولم يكن له كفوا أحد )لله قال لم يكن له شبيه ولا عديل, وليس كمثله شيء.

Ni Iymaan juu ya vile Alivyojisifu Allaah Mwenyewe katika Kitabu Chake, na jinsi alivyosifu Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na majina Yake Allaah na Sifa Zake tukufu, na kuamini kama yalivyokuja bila kujadili majina hayo na sifa hizo.

 

Kama vile Allaah Alivyothibitisha na Akakataza kuyajadili katika Qur-aan kwa kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

 يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا ﴿١١٠﴾

Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawawezi kufikia kuelewa chochote cha Ujuzi Wake. [Twaahaa: (20:110)]

 

Na kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ ﴿١١﴾

Hakuna chochote kinachofanana Naye. [Ash-Shuwraa: (42:11)]

 

Na kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yoteNaye Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri. [Al-An'aam: (6:103)]

 

Katika riwaayah ya At-Tirmidhiy kutoka kwa Ubayy bin Ka'ab (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba:

"Washirikina walimwambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale alipowataja miungu yao, walisema tutajie Mola wako kwa nasaha Na Allaah Akawateremshia Qur-aan kwa kuwaambia hivi: Waambie ee Rasuli ya kwamba:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾

Sema: Yeye Allaah Ni Mmoja Pekee.

اللَّـهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾

Allaah Aliyekamilika Sifa za Utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote. 

لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾

Hakuzaa wala Hakuzaliwa.

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾

 

Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye. [Al-Ikhlaasw: (112:1-4)

 

Na kwamba Mkusudiwa. “Hakuzaa wala Hakuzaliwa” hakuna kinachozaliwa isipokuwa kitakuwa na hakuna chenye kufa isipokuwa kitarithiwa, na Allaah, Hafi wala Kurithiwa.

“Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye”.

[Imepokewa na At-Tirmidhiy (3364), Ahmad (5/133), (134), Ibn Abi ‘Aswim katika As-Sunnah (663), Ibn Jariir At-Twabariy (15/342), Ibn Khuzaymah katika At-Tawhiyd (1/95), Al-Haakim (2/540) imesahihishwa na imewafikiwa na Adh-Dhahabiy, Al-Baihaqi katika Al-‘Iitiqaad uk 38, katika Al-Asmaa was-Swifaat (50), (608), Al-Bukhariy katika At-Tariykh (1/1/245), Ibn ‘Adiy (6/ 227), na Al-Waahidiy katika Asbaab An-Nuzuwl (947)].

 

 

Share