052-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Qur-aan na Sunnah Kuhusiana na Majina Yake Matukufu?

 

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

 

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

052-Ni Ipi Dalili Ya Qur-aan na Sunnah Kuhusiana na Majina Yake Matukufu?

 

 

 

Swali:

س: ما دليل الأسماء الحسنى من الكتاب والسنة

 

Ni Ipi Dalili Ya Qur-aan na Sunnah Kuhusiana na Majina Yake Matukufu?

 

Jibu:

ج: قال الله عز وجل( ولله الأسماء الحسنى فادعوه بها وذروا الذين يلحدون في أسمائه )وقال سبحانه( قل ادعوا الله أو ادعوا الرحمن أياما تدعوا فله الأسماء الحسنى )وقال عز وجل( الله لا إله إلا هو له الأسماء الحسنى )وغيرها من الآيات,

وقال النبي صلى الله عليه وسلم( إن لله تسعة وتسعين اسما من أحصاها دخل الجنة )وهو في الصحيح, وقال صلى الله عليه وسلم( أسألك اللهم بكل اسم هو لك سميت به نفسك ,أو أنزلته في كتابك أو علمته أحدا من خلقك أو استأثرت به في علم الغيب عندك أن تجعل القرآن العظيم ربيع قلبي )الحديث.

 

Ni kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa na kuharibu Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A'raaf: (7:180)].

 

Na kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ  ﴿١١٠﴾

Sema: Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. [Al-Israa: (17:110)]

 

Na kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ﴿٨﴾

Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Anayo Majina Mazuri kabisa. [Twaahaa: (20:8)]

 

Na nyinginezo.

 

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:  “Allaah ana majina tisini na tisa (99) na mwenye kuyahifadhi na kumuomba ataingia peponi”. [Imepokewa na Al-Bukhaariy (2736, 7392), Muslim (2677) Katika Hadiyth ya Abuu Huraiyrah]. Hadiyth Swahiyh.

 

Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

"Ee Allaah ninakuomba kwa kila jina Uliloliita Nafsi Yako, au Uliloshusha katika Kitabu Chako, au katika elimu Yako Uliompa yeyote katika viumbe Wako, au Ulilolichagua katika elimu Yako ya ghaibu na uifanye Qur-aan kuwa ndio muongozo wa moyo wangu”. [Imepokewa na Ahmad (1/391, 452), Ibn Hibaan (972), Abuu Ya'ala (5297), Al-Haakim (1/509), imesahihishwa na Al-Albaniy katika As-Swahiha (199)].

 

 

 

Share