01-Tukumbushane: Khatima Mbaya

 

 Tukumbushane

 

Alhidaaya.com

 

 

01:  Khatima Mbaya:

 

Madhambi ni daraja la kukupeleka kwenye mwisho mbaya wakati wa kufa, kwa kuwa mwanadamu anakufa kwa mujibu wa alivyoishi.  Hivyo basi, anayetaka kufa akiwa kwenye sijdah, basi akithirishe kusujudu kwa kuswali Swalah za Faradhi na za Sunnah.  Na anayetaka kufa hali ya kuwa yuko kwenye swawm, basi akithirishe sana kufunga.

 

Lakini kiufupi, khatima njema ni mtu kufa akiwa na tawhiyd safi bila kuwa na chembe ya shirki katika moyo wake vyovyote afavyo hata akifia barabarani.  Si lazima afie msikitini, au ameshika Msahafu na kadhalika.  Rasuli Mbora wa viumbe alifia kitandani.

 

Na yeyote mnayemwona anafia kwenye maasia, basi jueni huyo alipetuka mipaka dhidi ya nafsi yake katika maisha yake, na kwa sababu hiyo akanyimwa tawfiyq ya kufa kifo chema.

 

 

 

Share