02-Tukumbushane: Mali Ni Neema

 

Tukumbushane

 

Alhidaaya.com

 

 

02:  Mali Ni Neema:

 

 

Mali ni neema.  Kwa nini?  Kwa sababu Allaah ‘Azza wa Jalla Amekupa mali uliyonayo ili ununulie Pepo.

 

"إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ "

 

“Hakika Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata Jannah”.  [At-Tawbah: (111)].

 

‘Uthmaan bin ‘Affaan alifahamu maana hii akanunua Jannah mara mbili.  Mara ya kwanza alipomsikia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:

 

"مَن جَهَّز جَيشَ العُسرةِ فلَه الجَنَّةُ"

 

“Atakayeliandaa jeshi la Al’Usrah (kwa wanyama na zana) basi ataipata Pepo”. [Swahiyh Al-Bukhaariy]

 

Hivi ni Vita vya Tabuk, na jeshi limeitwa Al-‘Usrah kutokana na hali ngumu na ya dhiki iliyokuwepo wakati huo.  Hapo ‘Uthmaan akatoa mali yake yote.

 

Na mara ya pili ni pale alipomsikia Rasuli  (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:

 

"مَن حَفَر رُومةَ فَلَهُ الجَنَّةُ"

 

“Atakayechimba kisima cha maji, basi ataipata Jannah”.  [Swahiyh Al-Bukhaariy]

 

‘Uthmaan akanunua kisima cha maji kilichokuwa kinamilikiwa na mtu ambaye alikuwa akiuza maji yake.  Na hapa ni wakati Muhaajiruna walipokuwa wanahamia Madiynah ambapo mahitaji ya maji yangeongezeka.  Akakifanya kisima hicho ni waqf kwa ajili ya Allaah.

 

Hivyo chochote hata kidogo utoacho kwa mujibu wa hali yako basi usikidharau. Allaah ndiye ajuaye hali yako na nia yako.  Na haya ndiyo matumizi chanya ya utumiaji wa neema ya mali kwa mambo yote yenye kumridhisha Allaah.

 

                                                   

Share