01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Posa Na Hukumu Zake:Taarifu Na Hukmu Yake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الخِطْبَةُ وأَحْكَامُهَا

 

Posa Na Hukumu Zake

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

01:  Taarifu Na Hukmu Yake:

 

"الخِطْبَةُ" kwa kutia “kasrah” kwenye “khaaun”, ni ombi la kutaka kumwoa mwanamke.  Ikiwa ombi litakubaliwa, basi linageuka na kuwa ni ahadi ya ndoa, lakini haimaanishi kwamba ndoa ishafungika, bali mwanamke ataendelea kuwa ni ajnabiyya (mwanamke wa kando) kwa mpeleka posa huyo mpaka pale ndoa itakapofungwa na kuwa ni mkewe.

 

Hukmu Yake:

 

Posa si sharti ya kuswihi kwa ndoa.  Kama ndoa itafungwa bila kuwepo posa, basi ndoa hiyo ni sahihi, kwa kuwa aghalabu posa inakuwa ni njia ya kufikia kwenye nikaah.  Kwa upande wa Jumhuwr ya ‘Ulamaa, posa ni jambo lenye kujuzu kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa: 

 

"وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ"

 

“Wala si dhambi juu yenu katika ambayo mmedokezea ya kuposa wanawake”.  [Al-Baqarah: 235]

 

Ama kwa ‘Ulamaa wa Kishaafi’iy, ni jambo linalopendeza kutokana na alivyofanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomposa ‘Aaishah bint Abiy Bakr na Hafswah bint ‘Umar.

 

Mchakato huu utakwenda ikiwa hakuna kizuizi chochote kwa mwanamke kuolewa.  Na kama kipo, basi posa haifai.

 

 

Share