01-Majini: Majini Ni Akina Nani

 

 

Majini  

 

Alhidaaya.com 

 

 

 01- Majini Ni Akina Nani

 

 

 

Neno  "الجِنُّ" limenyambuliwa toka neno "الاجْتِنَانُ" lenye maana ya kufichika na kutoweza kuonekana.  Na kwa vile wanadamu hawawezi kuwaona, ndio wakaitwa majini.

 

Majini hawa ni viumbe vyenye akili, vyenye utashi na vilivyokalifishwa na Allaah Ta’aalaa kutekeleza maamrisho Yake na kuacha makatazo Yake, na kesho akhera watahisabiwa matendo yao waliyoyafanya hapa duniani.  Wameumbwa kutokana na moto, wana uwezo wa kujiweka katika maumbo tofauti, wanakula, wanakunywa, wanaoana na wanazaana kama sisi wanadamu.  Kwa hiyo basi, wana familia, watoto, wajukuu na kadhalika.    
 

Ibn Hazm amesema kuhusu majini:  “Ni umma wenye akili na utambuzi, wanafanya ‘ibada, wameahidiwa kulipwa mema kama watafanya mema, na adhabu kama  watakengeuka, wanazaana na wanakufa.  Asili yao ni moto kama ilivyo asili yetu sisi udongo”.

 

 

 

Share