02-Majini: Dalili Za Uwepo Wa Majini Toka Kwenye Qur-aan

 

 

Majini

 

   

Alhidaaya.com 

 

 

02-  Dalili Za Uwepo Wa Majini Toka Kwenye Qur-aan:

 

 

Allaah Ta’aalaa Amewataja majini sehemu mbalimbali katika Kitabu Chake Kitukufu.  Kati ya sehemu hizo ni:

 

1-  Suwrat Al-Jinn:

 

"قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا"

 

“Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم):  Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza, wakasema:  Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu”.  [Al-Jinn:  01]

 

As-Sa’adiyy amesema kuhusu suwrah hii:  “Ndani ya suwrah hii kuna faida nyingi.  Miongoni mwazo ni uwepo wa majini, na kwamba majini hawa wamekalifishwa mambo ya kufanya na mambo ya kuacha, na watakuja kulipwa matendo yao kama aya za suwrah hii zinavyoonyesha”.

 

2-  Suwrat Adh-Dhaariyaat:

 

"وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ"

 

Na Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa wapate kuniabudu Mimi tu”.  [Adh-Dhaariyaat:  56]

 

3-  Suwrat Al-An’aam:

 

"يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا"

 

“Enyi hadhara ya majini na wana Aadam!  Je hawajakufikieni Rusuli miongoni mwenu wanakusimulieni Aayaat Zangu na wanakuonyeni kukutana na Siku yenu hii?”  [Al-An’aam:  156]

 

4-  Suwrat As Sajdah:

 

"وَلَوْ شِئْنَا لَآتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَاهَا وَلَـٰكِنْ حَقَّ الْقَوْلُ مِنِّي لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ"

 

Na Tungelitaka, Tungeliipa kila nafsi mwongozo wake, lakini imethibiti kauli kutoka Kwangu kwamba:  Bila shaka Nitajaza Jahannam kwa majini na watu pamoja”.  [As-Sajdah:  13]

 

Ibn Jariyr amesema:  “Jahannam itajazwa majini na wanadamu waliomwasi Allaah”. 

 

Kwa maana kwamba majini nao wataingia motoni kutokana na matendo yao mabaya kama ilivyo kwa wanadamu.

 

5-  Suwrat Ar Rahmaan:

 

"فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ"

 

Mna humo wanawake wenye staha wanaoinamisha macho, hajawabikiri kabla yao binadamu yeyote wala jinni”.  [Ar-Rahmaan:  56]

 

Al-Baghawiy kasema:  “Hii ni dalili kwamba jini anajimai kama anavyojimai mwanadamu”. 

 

6-  Suwrat Al-Israa:

 

"قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا"

 

Sema:  Ikiwa watajumuika wana Aadam na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan; hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao”.  [Al-Israa: 88]

 

7-  Suwrat Sabaa:

 

"فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ الْجِنُّ أَن لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ الْغَيْبَ مَا لَبِثُوا فِي الْعَذَابِ الْمُهِينِ "

 

“Basi alipoanguka, ikawabainikia majini kwamba lau wangelikuwa wanajua ya ghayb, basi wasingelibakia katika adhabu ya kudhalilisha”.  [Sabaa: 14]

 

 

Share