066-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Yake Kutoka Sunnah?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
066-Ni Ipi Dalili Yake Kutoka Sunnah?
Swali:
س: ما دليل ذلك من السنة
Ni Ipi Dalili Yake Kutoka Sunnah?
Jibu:
ج: أدلته من السنة كثيرة لا تحصى, منها قوله صلى الله عليه وسلم في حديث الأوعال( والعرش فوق ذلك والله فوق العرش وهو يعلم ما أنتم عليه )وقوله لسعد في قصة قريظة "لقد حكمت فيهم بحكم الملك من فوق سبعة أرقعة" وقوله صلى الله عليه وسلم للجارية( أين الله )قالت في السماء قال( اعتقها فإنها مؤمنة) وأحاديث معراج النبي صلى الله عليه وسلم وقوله صلى الله عليه وسلم في حديث تعاقب الملائكة( ثم يعرج الذين باتوا فيكم فيسألهم وهو أعلم بهم ) الحديث, وقوله صلى الله عليه وسلم( من تصدق بعدل تمرة من كسب طيب ولا يصعد إلى الله إلا الطيب )الحديث, وقوله صلى الله عليه وسلم في حديث الوحي( إذا قضى الله الأمر في السماء ضربت الملائكة بأجنحتها خضعانا لقوله كأنه سلسلة على صفوان )الحديث وغير ذلك كثير, وقد أقر بذلك جميع المخلوقات إلا الجهمية.
Dalili ni nyingi kupitia Sunnah miongoni mwa hizo ni: Hadiyth ya Al-Awal:
“Na 'Arshi ipo juu ya hiyo, na Allaah Yupo juu ya 'Arshi kwa sifa ya Ufalme Wake kutoka juu ya mbingu saba.” [Hadiyth dhaifu Imepokewa na Abu Dawuwd (4723), At-Tirmidhiy (3320), Ibn Majah (193) na Al-Hakim (2/500,501)]
Na Hadiyth ya kijakazi: Allaah Yupo Wapi? Akajibu yule kijakazi kwa kusema: Allaah Yupo juu ya mbingu.
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
“Muache huru huyo kijakazi kwa iymaan yake". [Imepokewa na Muslim (537), Malik katika Muwatwa (2/595), Ahmad (2/291) na Abu Dawuwd (3284)]
Na Hadiyth ya Miraaj, na kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na kupokezana Malaaika:
“Kisha wanapanda wale ambao wamelala kwenu, na Yeye Ana wauliza hali ya kuwa Anawajua zaidi.” [Imepokewa na Al-Bukhaariy (7429) na Muslim (632)]
Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Mwenye kutoa sadaka kiasi cha tende ya halali na kwake hakipandishwi isipokuwa kizuri.”. [Imepokewa na Al-Bukhaariy (7430, 1410) na Muslim (1014)]
Na Hadiyth ya Wahyi
“Allaah Anapohukumu jambo mbinguni, Malaaika hupiga mbawa zao kwa unyenyekevu kwa kauli Yake, kana kwamba ni mnyororo juu ya jiwe”.
Na zinginezo nyingi.
Viumbe vyote vimekiri na kuthibitisha isipokuwa kundi la Jahamiyyah.