067-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Kauli Ya Viongozi Wa Dini Miongoni Mwa Salaf Swaalih Katika Mas-ala Ya Kulingana (Kwake Allaah Kwenye 'Arsh) Istiwaa?

 

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

 

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

 

067-Ni Ipi Kauli Ya Viongozi Wa Dini Miongoni Mwa Salaf Swaalih Katika Mas-ala Ya Kulingana (Kwake Allaah Kwenye 'Arsh) Istiwaa?

 

 

 

 

Swali:

س: ماذا قال أئمة الدين من السلف الصالح في مسألة الاستواء 

 

Ni Ipi Kauli Ya Viongozi Wa Dini Miongoni Mwa Salaf Swaalih Katika Mas-ala Ya Kulingana (Kwake Allaah Kwenye 'Arsh) Istiwaa?

 

Jibu:

 ج: قولهم بأجمعهم رحمهم الله تعالى: الاستواء غير مجهول والكيف غير معقول والإيمان به واجب والسؤال عنه بدعة ومن الله الرسالة ,وعلى الرسول البلاغ وعلينا التصديق والتسليم, وهكذا قولهم في جميع آيات الأسماء والصفات وأحاديثها( آمنا به كل من عند ربنا )(آمنا بالله واشهد بأنا مسلمون ).

Tamko lao la pamoja ni: Istiwaa ipo, na kuuliza ikoje sio sahihi, na kuamini ni wajibu, na kuuliza ni uzushi na kwa Allaah Ndio kwenye muongozo, na ni juu ya Rasuli kufikisha, na ni juu yetu kukubali na kujisalimisha na hili ndilo tamko lao kuhusiana na Aayah zote zinazohusu majina ya Allaah na sifa Zake, pamoja na Hadiyth za Nabiy.

 آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ  ﴿٧﴾

Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Rabb wetu. [Aal-'Imraan: (3:7)]

آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ ﴿١١١﴾

Tumeamini na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu. [Al-Maaidah: (5:111)]

 

 

 

Share