068-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Qur-aan Juu Ya Uwezo Wa Nguvu Zake?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
068-Ni Ipi Dalili Ya Qur-aan Juu Ya Uwezo Wa Nguvu Zake?
Swali:
س: ما دليل علو القهر من الكتاب
Ni Ipi Dalili Ya Qur-aan Juu Ya Uwezo Wa Nguvu Zake?
Jibu:
ج: أدلته كثيرة منها قوله تعالى( وهو القاهر فوق عباده )وهو متضمن لعلو القهر والفوقية. وقوله تعالى( سبحانه هو الله الواحد القهار )وقوله تعالى( لمن الملك اليوم لله الواحد القهار )وقوله تعالى( قل إنما أنا منذر وما من إله إلا الله الواحد القهار )وقوله تعالى( ما من دابة إلا هو آخذ بناصيتها )وقول تعالى( يا معشر الجن والإنس إن استطعتم أن تنفذوا من أقطار السماوات والأرض فانفذوا لا تنفذون إلا بسلطان )وغير ذلك من الآيات.
Dalili ni nyingi, katika hizo ni kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
( وهو القاهر فوق عباده )
Naye Ndiye Mwenye nguvu juu ya waja Wake
Inaambatana na Uwezo wa nguvu Zake juu ya kila kitu.
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
سُبْحَانَهُ ۖ هُوَ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٤﴾
Subhaanah! (Utakasifu ni Wake), Yeye Ndiye Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Az-Zumar: (39:4)
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْمَ ۖ لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ﴿١٦﴾
Ufalme ni wa nani leo? (Allaah Mwenyewe Atajijibu): Ni wa Allaah Pekee Mmoja, Asiyepingika. [Gaafir: (40:16)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
قُلْ إِنَّمَا أَنَا مُنذِرٌ ۖ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٦٥﴾
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi ni mwonyaji tu. Na hakuna Muabudiwa wa haki yeyote isipokuwa Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Swaad: (38:65)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
مَّا مِن دَابَّةٍ إِلَّا هُوَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهَا ۚ ﴿٥٦﴾
Hakuna kiumbe chochote kitembeacho isipokuwa Yeye (Allaah) Ni Mwenye Kukamata hatamu za paji lake (Kukipeleka Atakavyo Yeye). [Huwd: (11:56)]
Na kauli ya Allaah (عزَّ وجلَّ):
يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَن تَنفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ فَانفُذُوا ۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَانٍ ﴿٣٣﴾
Enyi jamii ya majini na wanaadam! Mkiweza kupenya kwenye zoni za mbingu na ardhi, basi penyeni. Hamtoweza kupenya isipokuwa kwa mamlaka (ya Allaah). [Ar-Rahmaan: (55:33)]
Na zinginezo zaidi ya hizo.