01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mahari: Taarifu Yake Na Hukmu Yake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

 

الصَّدَاقُ

 

Mahari

 

Alhidaaya.com

 

 

01:  Taarifu Yake Na Hukmu Yake:

 

 

"الصَّدَاقُ"  katika istilahi, ina maana ya badali inayotolewa kwa ajili ya ndoa au mfano wake, ni sawa kwa kupangwa na mtawala, au kwa kuridhiana kati ya mke na mume.  Inaitwa pia "مَهْرٌ" , "أَجْرٌ"  na "فَرِيْضَةٌ" na kadhalika.

 

Sababu ya kuitwa "الصَّدَاقُ" , ni neno lenyewe kuhisisha ukweli wa utashi wa mwanaume kumwoa mwanamke.

 

 Mahari hii ni wajibu kwa mwanaume kwa sababu ya kuoa au kumuingilia mwanamke kwa mujibu wa ‘Ijmaa ya Ulamaa wa Kiislamu.  Uimara wa ‘Ijmaa hii hautiwi doa na Mahanafiy na Mashaafi’iy ambao wao wamejuzisha kutokuwepo mahari kwenye ndoa kama ilivyoelezwa nyuma.

 

Na nyuma ishaelezwa kwamba mahari ni sharti kwa ajili ya kuswihi kwa ‘aqdi ya ndoa, ni sawa mahari iliyobainishwa ikatajwa au ambayo haikubainishwa.  Mwanamke atapewa mahari mfano wake kwa mujibu wa kauli mbili za ‘Ulamaa zilizo sahihi zaidi.

 

 

 

Share