28-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Nakuusieni Taqwa Ya Allaah Na Usikivu Na Utiifu
Hadiyth Ya 28
أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللهِ والسَّمْعِ والطَّاعَةِ
Nakuusieni Kumcha Allaah Na Usikivu Na Utiifu
عن أبي نَجيحٍ الْعِرْباضِ بنِ سارِيَةَ رضي اللهِ عنه قال: وَعَظَنَا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنها الْقُلُوبُ، وذَرَفَتْ منها الْعُيُونُ، فَقُلْنا: يا رسول اللهِ، كأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ، فأَوْصِنا. قال: ((أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللهِ عَزَّ وَجَلَّ، والسَّمْعِ والطَّاعَةِ، وإن تَأَمَّرَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ، فإنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اخْتِلافاً كَثِيراً، فَعَليْكُمْ بِسُنَّتي وسُنَّةِ الخُلفَاءِ الرَّاشِدِينَ المَهْدِيِّينَ، عَضُّوا عَلَيْها بالنَّواجِذِ، وإيَّاكُمْ ومُحْدَثاتِ الأُمُورِ، فإنَّ كلَّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ وَ كُلَّ بِدْعَةٍ ضَلاَلَةٌ وَكُلَّ ضَلاَلَةٍ فِي النَّارِ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
Imepokelewa kutoka kwa Abu Najiyh Al-‘Irbaadhw bin Saariyah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitupa mawaidha mazito (yenye maana kubwa), nyoyo zikaogopa na macho yakabubujikwa machozi. Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Yanaonekana kama kwamba mawaidha ya kutuaga, basi tuusie. Akasema: “Nakuusieni kuwa na taqwa ya Allaah na usikivu na utiifu japokuwa mtaongozwa na mtumwa. Hakika atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona ikhtilaaf nyingi. Kwa hiyo, shikamaneni na Sunnah zangu na mwenendo wa Makhalifa waongofu, yashikilieni kwa magego (mambo yao). Na tahadharini na mambo yenye kuzushwa, kwani kila uzushi ni bid’ah, na kila bid-ah ni upotofu, na kila upotofu ni motoni.” [Abuu Daawuwd, AT-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]