29-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Muabudu Allaah Na Usimshirikishe Na Chochote

 

Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah:

 

Hadiyth Ya 29

 

تَعْبُدُ اللهَ لا تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً

 

Muabudu Allaah Na Usimshirikishe Na Chochote

 

Alhidaaya.com

 

Sikiliza Hadiyth:

 

 

 

عن معاذِ بن جبلٍ رضي الله عنه قال: قلت: يا رسول الله، أخْبِرني بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجنَةَ ويُبَاعِدُني عَنِ النارِ. قال: ((لَقَدْ سألْتَ عَنْ عَظيمٍ، وإنَهُ لَيَسيرٌ عَلى من يَسَّرَهُ اللهُ تعالى عَلَيْهِ: تَعْبُدُ اللهَ لا تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً، وتُقيمُ الصَّلاةَ، وتُؤتي الزكاةَ، وتصومُ رمضانَ، وتَحُجُّ البيتَ))

ثم قال:  ((ألا أَدُلُّكَ على أبْوَابِ الخيرِ؟: الصَّومُ جُنَّةٌ، والصَّدقةُ تُطْفِىءُ الخَطِيئةَ كما يُطْفىءُ الماءُ النارَ، وصَلاةَ الرَّجُلِ في جَوْفِ الَّليْلِ، ثم تلا: ((تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنْ الْمَضَاجِعِ)) حتى بلغ : ((يَعْمَلُونَ))  السجدة: 16-17 .

ثم قال:  ((ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأمْرِ وَعَمودِهِ وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ؟)) قلتُ: بَلىَ يا رسول الله. قال:  ((رَأْسُ الأمْرِ الإسلامُ، وعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الجِهادُ))

ثم قال: ((ألا أخْبِرُكَ بِمِلاكَ ذَلِكَ  كلِّهِ ؟)) فَقُلْتُ بَلَى يا رَسول الله، فأخَذَ بِلِسانِهِ وقال: ((كُفَّ عَلَيْكَ هذا)) قلت: يا نبيَّ الله، وإنَّا لمؤاخَذُونَ بِما نَتَكَلَّمُ بِه ؟)) فقال: (( ثَكِلَتْكَ أمُّكَ يَا مُعَاذُ،  وَهَلْ يَكُبُّ الناسَ في النارِ على وُجُوهِهِمْ))  أو قال: ((على مناخِرِهِم - إلاَّ حَصَائدُ  ألسِنَتهم))  رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ   وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ. 

 

Imepokelewa kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah, nijulishe ‘amali itakayoniingiza Jannah na itanibaidisha na moto. Akasema: “Umeniuliza jambo kubwa mno nalo ni jepesi kwa ambaye Allaah Ta’aalaa Amemwepesishia.  Muabudu Allaah usimshirikishe na chochote, na usimamishe Swalaah, na utoe Zakkaah, na ufunge swawm Ramadhwaan, na uhiji Nyumba (Makkah).” 

 

Kisha akasema: “Je nikuelekeze milango ya kheri? Swawm ni ngao, na swadaqah inazima madhambi kama vile maji yanavyozima moto, na Swalaah ya mtu katika nyakati za usiku.” Kisha akasoma:

((تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنْ الْمَضَاجِعِ))

 

 

Mbavu zao zinatengana na vitandaa..”

 

mpaka akafikia:

((يَعْمَلُونَ))

 

“wakiyatenda” [As-Sajdah: 16-17]

 

Kisha akasema: “Je, nikujulishe  kilele cha hilo jambo na nguzo yake na sehemu yake ya juu kabisa?”  Nikasema: Ndio ee Rasuli wa Allaah! Akasema:  “Kilele chake ni Uislamu, nguzo yake ni Swalaah na sehemu yake ya juu kabisa ni jihaad.”

Kisha akasema: “Je, nikujulishe muhimili wa yote haya?”  Nikasema:  Ndio ee Rasuli wa Allaah!  Akaukamata ulimi wake na akasema: “Uzuie huu!” Nikasema: Ee Nabiy wa Allaah! Kwani hivi sisi tutahukumiwa yale tunayoyasema?  Akasema: “Akukose mama yako ee Mu'aadh! 

Kuna kitu zaidi kinachowaangusha watu kifudifudi motoni?” 

Au kasema: “Juu ya  pua zao – isipokuwa ni ni mavuno ya ndimi zao?” [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]

Maana ya:

ثَكِلَتْكَ أمُّكَ

“Akukose mama yako”: Ni Neno linalotamkwa na Waarabu katika hali ya kukemea bila ya kukusudiwa maana yake.

 

 

 

 

Share