30-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Allaah Amefaridhisha Mambo Ya Kuwajibika Basi Msiyapoteze
Hadiyth Ya 30
إنّ اللهَ تَعَالى فَرَضَ فَرَائِضَ فَلاَ تُضَيّعوها
Hakika Allaah Amefaridhisha Faraaidhw
(Mambo Ya Kuwajibika Katika Dini) Basi Msiyapoteze
عَنْ أَبيِ ثَعْلَبَةَ الخُشَنِيِّ جُرْثُومِ بْن نَاشرٍ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إنّ اللهَ تَعَالى فَرَضَ فَرَائِضَ فَلاَ تُضَيّعوهاَ وَحَدَّ حُدُودَاً فَلاتَعْتَدُوهَا وَحَرّمَ أَشْياءَ فَلاَتَنْتَهِكُوهَا وَسَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ رَحْمَةً لَكُمْ غَيْرَ نِسْيانٍ فَلا تَبْحَثُوا عَنْهَا)) حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ الدَّارَقُطْنِيّ وَغَيْرُهُ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Tha'alabah Al-Khushaniyy Jurthuwm bin Naashir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ”Hakika Allaah Amefaridhisha faraaidhw (Mambo ya kuwajibika katika Dini) hivyo msiyapoteze. Na Akaweka mipaka basi msiivuke. Na Ameharamisha mambo kwa hivyo msiyahalifu. Na Amenyamazia mambo kutokana na rahmah (Yake) kwenu wala hakusahau kwa hivyo msiyadadisi.” [Hadiyth Hasan Ad-Daaraqutwniy na wengineo]