31-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Ipe Mgongo Dunia Allaah Atakupenda
Hadiyth Ya 31
ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ
Ipe Mgongo Dunia Allaah Atakupenda
عَنْ أَبِي العَبّاسِ سَهلِ بْن سَعْدٍ السّاعِدِيِّ رضي الله عنه قَالَ : جَاءَ رَجُلُ إِلى النَبِي صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أَحَبَّنِي اللَّهُ وَأَحَبَّنِي النَّاسُ . فَقَالَ: (( ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبُّكَ النّاسُ)) رَوَاهُ ابْنُ مَاجَهْ وَغَيْرُهُ بِأَسَانِيدَ حَسَنَةٍ.
Imepokelewa kutoka kwa Sahl bin Sa'ad As-Saa’idiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: “Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Nijulishe ‘amali ambayo nikiifanya Allaah Atanipenda na watu pia watanipenda. Akasema: “Ipe mgongo dunia Allaah Atakupenda, na vipe mgongo vilivyomo kwa watu, watu watakupenda.” [Ibn Maajah na wengineo kwa mtiririko mzuri wa isnaad]*
*Hata hivyo Wanavyuoni wa Hadiyth wameeleza kuwa Hadiyth hii ni dhaifu kutokana na udhaifu wa sanad yake japo An-Nawawiy kaitumia na kasema ina sanad nzuri.