27-Dalili Za Kheri Katika Mambo Yamfaayo Maiti: Kuoshwa maiti upesi
Kuoshwa maiti upesi:
Katika mambo ya kheri ambayo humfikia maiti ni kufanya upesi katika kumtayarisha kwa kumkosha, kumkafini na kumzika.
Katika kuoshwa vinachungwa vifuatavyo:
· Idadi ya kuoshwa iwe ni mara tatu na zaidi ikibidi kwa haja kwa sharti kuwa idadi hiyo iwe ni witri: tatu, tano au saba na mfano wa haya.
· Itumike majani ya mkunazi au sabuni katika kila anapokoshwa ili kumsafisha vizuri zaidi.
· Muoshaji atumie sabuni au mfano wake kama vile siku hizi gloves inavyotumika na kuwepo na sitra yenye kumfunika maiti baada ya kuvuliwa nguo.
· Ni vizuri kutia kafuri katika maji haswa katika josho la mwisho au mafuta mazuri maadamu sio haramu, na inapokuwa ni haramu basi hayafai.
· Kucha za mwanamke zitapunguzwa na kuoshwa vizuri, hali kadhalika nywele zake kuchanwa na kufungwa vifundo vitatu nyuma yake.
· Aanze kukosha sehemu za kulia kwanza na sehemu za udhu
· Mwanamume hukosha wanaume, mwanamke hukosha wanawake, mume humuosha mkewe na mke humkosha mumewe.
· Shahidi, aliyekufa katika vita hakoshwi.