28-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Waliymah (Karamu) Ya Ndoa Inaweza Kuwa Chochote Bila Ya Nyama

 

 

Inaruhusiwa kufanya karamu ya ndoa kwa chakula chochote kinachopatikana na kwa uwezo hata kama sio pamoja na nyama. Hii ni kutokana na Hadiyth ifuatayo iliyosimuliwa na Anas:

 

أَقَامَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بَيْنَ خَيْبَرْ وَالْمَدِينَة ثَلاثَ لَيَالٍ يبني عَلَيْهِ بِصَفِيَّة، فدَعوتُ المسلمينَ إلى وَلِيمَتِهِ، فَمَا كَانَ فِيهَا مِنْ خُبْزٍ وَلاَ لَحْمٍ وما كان فيها إلاّ أن أمرَ بلالاً بالأنطاع فبُسطَت،  (وفي رواية) : فَحصت الأَرْض أَفَاحِيص، وَجِيءَ بِالأنْطاَع فَوَضَعت فِيهَا ) ، فَألْقَي عَلَيْهَا التَّمر وَالأَقطْ والسَّمْن [فَشَبَعَ النَّاسُ] 

"Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikaa baina ya Khaybar na Al-Madiynah kwa muda wa siku tatu siku ambazo alimuingilia (alimuoa) Swafiyah. Kisha nikawaalika Waislamu katika karamu yake ya ndoa. Hakukuwa na nyama wala mikate katika karamu, bali matandiko ya ngozi yaliletwa na juu yake zikawekwa tende, maziwa makavu na samli iliyo safi. Watu walikula hadi wakashiba"[1]

 

 

 



[1] Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo

Share