29-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Matajiri Kuchangia Gharama Za Karamu
Inapendekezeka kwa matajiri kusaidia katika matayarisho ya karamu ya ndoa kutokana na Hadiyth iliyosimuliwa na Anas kuhusu ndoa ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwa Swafiyah:
حتى إِذا كان بالطريقِ جَهَّزَتْها له أمُّ سُليمٍ فأهدَتْها له منَ الليل، فأصبحَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم عَروساً، فقال: ((مَن كان عندَه شيءٌ فليجىءْ به)) ( وفي رواية) ((من كان عنده فضل زاد فليأتنا به)) قال: وبَسطَ نِطعاً فجعلَ الرجلُ يجيءُ بالأقط، وجعلَ الرجلُ يجيءُ بالتمرِ، وجعلَ الرجلُ يجيءُ بالسَّمنِ فحاسوا حَيساً، (فجعلوا يأكلون من ذلك الحيس ويشربون من حياض إلى جنبهم من ماء السماء) فكانتْ وَليمةَ رَسولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم
"Kisha tulipokuwa njiani, Ummu Sulaym alimtayarisha (Swafiyah) kwa ajili yake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم na akamletea usiku. Kwa hiyo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliamka asubuhi na bibi harusi mpya. Kisha akasema: ((Yeyote mwenye kitu alete)). Katika riwaaya nyingine alisema, ((Yeyote mwenye riziki zaidi alete)). Anas anaendelea (kusema): Kwa hiyo matandiko ya ngozi yakatandikwa na mtu mmoja alileta maziwa makavu, mwingine tende, na mwingine samli