33-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kufungua Swawm Kwa Ajili Ya Mwenyeji (Aliyekualika)

 

 

Mtu (aliyefunga) anaweza kufungua Swawm ikiwa ni Swawm ya Sunnah, haswa ikiwa mwenyeji wake amemuomba kufanya hivyo. Kuna Hadiyth mbali mbali kuhusu mas-ala haya:

 


Kwanza:

((إِذَا دُعِيَ أَحَدُكُمْ إِلَى طَعَامٍ فَلْيُجِبْ فَإِنْ شَاءَ طَعِمَ، وَإِنْ شَاءَ تَرَكَ))

 

((Mmoja wenu anapoalikwa chakula, ahudhurie, kisha akitaka kula anaweza kula na kama sivyo anaweza kuacha))[1]

 


Pili:

((الصَّائِمُ المتطوِّعُ أَمِيرُ نَفْسِهِ إِنْ شَاءَ صَامَ، وَإِنْ شَاءَ أَفْطَرَ))

((Mwenye kufunga (Swawm za) Sunnah, ni mwenye kujitawala humo (katika Swawm) akipenda akamilishe Swawm yake au akipenda afungulie))[2]





Tatu:

عن عائشة رضي الله عنها  قالت : دَخَلَ عَليَّ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَوْماً فَقَالَ: ((هَلْ عِنْدَكُمْ شَيْءٌ؟)) فَقُلْتُ: لاَ قَالَ: ((فَإنِّي صَائِمٌ)) ثُمَّ مَرَّ بِـــــي بَعْدَ ذٰلِكَ الْيَوْمَ وَقَدْ أُهْدِيَ إلَى حَيْسٌ فَخَبَّأْتُ لَهُ مِنْهُ وَكَانَ يُحِبُّ الحَيْسَ قَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إنَّهُ أُهْدِيَ لَنَا خَيْسٌ فَخَبَّأْتُ لَكَ مِنْهُ قَالَ: ((أَدْنِيهِ أَمَا إِنِّي قَدْ أَصْبَحْتُ وَأَنَا صَائِمٌ)) فَأَكَلَ مِنْهُ ثُمَّ قَالَ: ((إنَّمَا مَثَلُ صَوْمِ الْمُتَطَوِّعِ مَثَلُ الرَّجُلِ يَخْرِجُ مِنْ مَالِهِ الصَّدَقَةَ فَإنْ شَاءَ أَمْضَاهَا وَإنْ شَاءَ حَبَسَهَا))  

Imetoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah الله عنها رضي ambaye amesema: "Mjumbe wa Allaah alinijia siku moja na akasema, ((Je kuna chochote? [chakula?])) Nikasema: Hapana. Akasema:  ((Nimefunga)). Kisha akaja kwangu siku nyingine na wakati huo nilikuwa nimeletewa Hais, kwa hiyo nikamuwekea kwani alikuwa akipenda Hais. Mama wa waumini ‘Aaishah akasema, "Ewe Mjumbe wa Allaah, nimegaiwa Hais na nimekuwekea baadhi". Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم Akasema: ((Ilete, nimeanza siku kwa kufunga)). Kwa hiyo akala baadhi yake na akasema: ((Swawm ya hiari (Ya Sunnah) ni mfano kama mtu anayetoa sadaka kutoka mali yake. Akipenda anatoa na asipopenda anazuia))[3]



[1] Muslim, Ahmad na wengineo

[2] An-Nasaaiy katika 'Al-Kubraa', Al-Bayhaaqiy na Haakim: Swahiyh

[3] An-Nasaaiy: Swahiyh

Share